Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto) akitoa maelezo ya utangulizi wakati wa ufunguzi wa kikao cha Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri (CHMT) kikijadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha kwanza kilifanyika leo Machi 25, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni mgeni rasmi aliyekaribishwa kufungua kikao hicho, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna (katikati) na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale (kulia).
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, Jerry Mwakanyamale (Kulia) akiongea wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna (Katikati) katika ufunguzi wa kikao cha Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri (CHMT) kikijadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha kwanza kilifanyika leo Machi 25, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna (katikati) akifungua kikao cha Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri (CHMT) kikijadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika mfumo wa afya ya Jamii mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Pembeni kushoto ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale na Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto). Kikao hicho cha kwanza kilifanyika leo Machi 25, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Wajumbe wa Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) wakifuatilia kwa makini.
Wajumbe wa Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) wakifuatilia kwa makini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...