Wahamiaji Haramu hao walikamatwa juzi katika kitongoji cha Gezaurole katika kata ya Ruaha Mbuyuni tarafa ya Mahenge wakati jeshi la polisi likiwa katika doria ya kawaida na kulitilia mashaka gari hilo lililokuwa limebeba matenga ya Nyanya.
 Kiongozi wa Wahamiaji Haramu,akiwagawia wenzake mikate  ilionunuliwa na wanahabari waliokuwepo kwenye tukio hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani humo.
 Kiongozi wa Wahamiaji Haramu,akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na sakata lao la kukamatwa nchini Tanzania,anasema wamesafiri nchini kwao Ethiopia mpaka Tanzania kwa siku 21 
 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akizungumza na Waaandishi wa habari mapema leo mchana,kwenye makao ya Polisi ya mkoani humo,akithibisha kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao wakiwa katika roli lenye usajili wa namba T 342 AJU likiwa linaendeshwa na dereva Mbega Ally (37) mkazi Tanga wakitokea nchini Ethiopia kuelekea nchini Afrika Kusini.
 Roli lenye usajili wa namba T 342 AJU likiwa linaendeshwa na dereva Mbega Ally (37) mkazi Tanga ndilo lililotumika kuwabeba wahamiaji hao.
 Matenga ya Nyanya ambamo Wahamiaji hao walikuwa wamekaa.PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-IRINGA
=======  =======  ======

WAHAMIAJI HARAMU 46 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI

Na Denis Mlowe,Iringa

JESHI la Polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 46 kutoka Ethiopia waliokuwa wakielekea nchini Afrika ya Kusini.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi amethibitisha kukamatwa wahamiaji hao wakiwa katika roli lenye usajili wa namba T 342 AJU likiwa linaendeshwa na dereva Mbega Ally (37) mkazi Tanga..

Mungi alisema wahamiaji hao walikamatwa juzi katika kitongoji cha Gezaurole katika kata ya Ruaha Mbuyuni tarafa ya Mahenge wakati jeshi la polisi likiwa katika doria ya kawaida na kulitilia mashaka gari hilo.

“Jeshi la polisi lilipata habari za kiintelejensia kuwa kuna roli limebeba wahamiaji haramu vijana wakajipanga na kufanikiwa kuwakamata wakiwa katikakati matenga ya nyanya yaliyopangwa kwa pembeni na na kufanikiwa kuwakamata vijana hao 46 akiwemo mtoto wa miaka 17” alisema Mungi.

Alisema kuwa dereva wa gari hilo anashikiriwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi na kusema baadhi ya Waethiopia hao 6 kati yao wana hati ya kusafiria (passport).

Katika hali kuonyesha ukarimu kwa wageni hao haramu waandishi wa habari walioko katika kampeni za jimbo la Kalenga wa mkoa wa Iringa na nje ya mkoa waliwapatia msaada wa vyakula wahamiaji hao baada ya kuonyesha wanakabiliwa na njaa kali na kiu ya maji.

Waandishi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa Iringa (IPC), Frank Leonard walichangishana na kupatikana kiasi cha shilingi elfu 50 na kufanikiwa kuwapatia vyakula hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Wanatafuta maisha.Inaonekana wana hali mbaya sana kiafya nadhani muhimu kwanza nikupewa huduma.Ulaya wanahifadhiwa hawadhalilishwi kama hivi.Mungu awasaidie.Hakuna anaependa kukimbia nchi yake.Ni shida ya maisha ,vita nk.Wapewe huduma kwanza ni muhimu.

    ReplyDelete
  2. Kwani mgewaacha wakaenda huko SA mngepungukiwa nini? Ili mradi hawaweki kambi nchini kwetu.

    ReplyDelete
  3. Mababu zetu wa millennia zilizopita watatucheka na kutushangaa sana kama wana wa Afrika tunabaguana na kuwaita ndugu zetu "HARAMU"!! Hapa kuna tatizo vuchwani mwetu! Hata Robert Nester Marley atashangaa kuona miaka zaidi ya 50 ya "kujitawala" bado Afrika imegawanyika vipande vipande kwa mistari iliyochorwa kule Ulaya!! Hakuna cha kujivunia uAfrika wangu kama mambo haya yanaendelea!

    ReplyDelete
  4. Ukipita nchi ya watu ama kuingia bila kufuata taratibu ndiyo haramu hiyo. Hilo dogo. Kubwa ni kwamba hii biashara inaitwa human trafficking.

    Ni biashara inapigiwa vita kote duniani. Wengi wamepoteza maisha katika mazingira kama hayo ya kufungiwa kwenye makasha kama nyanya.

    Najiuliza huko Ethiopia wako wananchi wangapi. Kila wiki wanakamatwa! Je hawajaisha huko kwao? Wanahama nchi?

    ReplyDelete
  5. wewe msemaji hapo juu, ukitaka kujua raha nenda nchini mwao uingie bila passport uone watakufanya kitu gani.

    lazima sheria za kimataifa zifuatwe, Tanzania siyo shamba la kuvuna migagi.

    ReplyDelete
  6. Hao jamaa wangeachwa waendelee na safari ayao,tena Waethiopia hawana matatizo ya ugaidi na uhalifu,ni watu tu wanahangaika kutafuta maisha kutokana na ukali wa maisha na njaa nchini mwao,Kama binadamu na ni waafrika wenzetu inafaa wapewe huduma zifaazo om chakula na malazi ya kawaida ili waweze kuendelea na safari yao,maana tunajua Iringa kuna bariadi kalai wasije wakaugua neomonia bure,wanaonekana siyo wahalifu wa kudhuru nchi yetu.

    ReplyDelete
  7. Hawakatazwi kusafiri ama kuondoka eneo jingine kwenda kwingine, CHA MUHIMU NI KUSAFIRI KWA KUFUATA SHERIA KAMA KUTUMIA PASIPOTI NA KUINGIA NCHI HADI NCHI KWA KUTUMIA VIZA.

    HIVYO KWA KITENDO CHAO CHA KUSAFIRI BILA UTARATIBU UNAOKUBALIKA WA KUTUMIA PASIPOTI NA VIZA NDIO KILICHO WAFANYA WAWEKWE CHINI YA SHERIA HATA KAMA WALIKUWA WANAPITA NJIA TANZANIA KWENDA HUKO KUSINI MWA AFRIKA.


    Ustawi wa Utaifa ni muhimu ktk Maendeleo ndio mana rtunajipanga kwa misingi ya nchi.

    Lazima tuishi duniani kwa kufuata Kanuni na Sheria na sio kusingizia Uafrika na Haki za Binaadamu kwa kutaka Kusafiri bila kufuata taratibu!!!

    ReplyDelete
  8. Waethiopia ndugu zetu Afrika ni moja na na wala Afrika siyo msitu, hamkatazwi kusafiri lakini mtumie taratibu zinazotakiwa hakuna atakaye wakamata!

    Mfano ktk Kundi lenu la watu 46 wenzenu 6 wanazo Pasipoti lakini ni kwa nini wasizitumie kusafiria?

    Badala yake Waethiopia mkubali kurundikwa na Mgosi wa Kaya Mbega wa Tanga kwenye Lori la Fuso?

    ReplyDelete
  9. 1. Kweli kuwekwe system/utaratibu wa kupita nchi yetu...kimya kimya...tufuate ile " Don't Ask, Don't Tell" yaani tujifanye hatuwani wanavyopita - ila tuhakikishe WANAPITA....
    2. Dreva/Mpangaji safari alichemsha ndio maana gari limeshtukiwa. utabebaje NYANYA kutioka Tanga unapita mkoa wa Iringa ? hapo karibu walipokamatwa (karibu na ILULA) Nyanya zinazalishwa zinaenda Dar na Northern TZ mpaka Nairobi! walichagua wrong product ku-camoflage. Angebeba matenga ya NAZI angepita...

    ReplyDelete
  10. Wanaokamatwa ni wasio na hela tu. Wenye mshiko saa hizi wana pasi na uraia wa Tz! kama magabacholi wanvyopewa urai na hakuna vyo vinavyoweza kuchunguza kama wamesitisha uraia wao wa awali. Mtawafanya nini hawa sasa, warudisheni kwao basi!

    Mnyonge

    ReplyDelete
  11. JAMANI ETHIOPIA KUNA MATATIZO GANI? JUZI KUNA MMOJA ALIKIMBIA NA NDEGE HUKO KWAO!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...