Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi. 
 MWANARIADHA wa Kitanzania, Jackline Sakilu jana aliibuka shujaa katika mashindano ya mbio ndefu za kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2014, baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya kilomita 21, (nusu marathon), kwa upande wa wanawake. 
 Katika mbio hizo zilizofanyika mjini Moshi,Sakilu ambaye ni afisa wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) amefanikiwa kuvunja rekodi iliyowekwa na mshindi wa kwanza wa mwaka jana ,Sara Ramadhan ya saa 1:13.05 baada ya kufanikiwa kumaliza mbio kwa kutumia saa 1:12:43 mbele ya wanariadha kutoka nchi jirani ya Kenya. 
 Kutokana na ushindi huo Sakilu amefanikiwa kujinyakulia medali ya dhahabu na kitita cha fedha taslimu kiasi cha sh Milioni 4 baada ya kuwabwaga wenzake wakiwemo Wakenya ambao hata hivyo wameendelea kutawala mbio hizo . 
 Nafasi ya pili ilienda kwa Mwanariadha Cynthia Towett wa klabu ya Michezo ya Nairobi aliyekimbia akitumia muda wa saa 1:14:33,na kujihakikishia zawadi ya medali ya shaba na kitita cha sh Mil 1 huku nafasi ya tatu ikichukulna na mkenya mwenzake Naomi Maiyo aliyetumia saa 1:17:47 na kujinyakulia medali ya fedha na kitita cha shilingi 500,000. 
 Hata hivyo wakenya waliendeleza ubabe wao, baada ya wanariadha wake kushika nafasi ya kwanza katika mbio za kilomita 42 na kilomita 21 wanaume, pamoja na nafasi ya kwanza katika kilomita 42 upande wa wanawake. 
 Mwanariadha Alfred Lagat alijihakikishia nafasi ya kwanza kwa mbio za nusu marathoni wanaume akikimbia kwa muda wa saa 1:02:34 akifuatiwa na Wakenya wenzake Silah Limo (1:03:04) na Keneth Kandie (1:03:20) huku Mtanzania wa pekee katika kumi bora, Alfred Felix, kutoka Klabu ya riadha ya Holili (HYAC) akishika nafasi ya tano (1:03:27). 
 Kwa upande wa mbio za Km 42 mshindi wa kwanza David Ruto kutoka Kenya alitumia muda wa saa 2:16:04,akiwashinda wakenya wenzake Julius Kilimo aliyetumia saa 2:16:17 akishika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Victor Serem aliyetumia saa 2:16:32 . 
 Mtanzania pekee aliyefanikiwa kuingia katika kumi bora katika mbio hizo ni Daudi Lwabe aliyemaliza mbio kwa kutumia muda wa saa 2:18:34 na kushika nafasi ya 8. Kilometa 42 kwa upande wa wanawake kwa mara nyingine wakenya wameendelea kushika nafasi za juu baada ya mshindi wa nafasi ya tatu katika mbio za mwaka jana Frida Lodera wa klabu ya michezo ya Nairobi kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kutumia muda wa saa 2:40:11, nafasi ya pili Joan Rotich (2:42:46) huku nafasi ya tatu ikishikwa na Abigal Toroitich akitumia muda wa saa 2:55:14. 
 Mwanariadha maarufu nchini Banueria Bryton alifanikiwa kuingia katika kumi bora baada ya kuhitimisha mbio akitumia muda wa saa 3:12:26.
Waziri wa habari, Utamaduni na Michezo Dk Fenera Mukangara akikabidhi mfano wa hundi ya sh Milioni  2 kwa mshindi wa pili wa  Half Marathoni wanawake.
Washindi wa Half Marathoni wakiwa katika picha ya pamoja.
Mshindi wa kwanza wa Full Marathoni David Ruto kutoka Kenya akionesha mfano wa hundi ya sh mil 4 iliyotolewa kwa mshindi wa kwanza.
Wadau wakiwa katika maadalizi ya mbio za Vodacom Fun Run.
Kwa picha zaidi na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...