Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Job Ndugai .

(Na Jovina Bujulu, MAELEZO DODOMA).
 
Muungano wa Tanzania bara na Zanzibar ni jambo la kujivunia kwa watanzania wote na katika bara la Afrika.

Hayo yamesemwa leo na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Job Ndugai wakati wa mahojiano katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha TBC ONE.

Mh. Ndugai ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema kuwa jambo la Muhimu tunalotakiwa kufanya kwa sasa ni kuimarisha na kuboresha Muungano ili tuweze kupiga hatua za kimaendeleo.

“Hatuna budi kuendelea kuuimarisha muungano uliopo ikiwa ni kichocheo cha maendeleo, tumeona mifano kwenye nchi kadha wa kadha zilizo katika muungano mfano nchi Marekani imekuwa mfano bora duniani kimaendeleo hasa kutokana na Muungano uliopo” Alisema Ndugai.

Mh. Ndugai aliongeza kuwa hata Muasisi wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akitukumbusha mara kwa mara kuusimamia muungano wa Tanzania na kuudumisha.

“Muasisi wa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akiasa Watanzania wote kuudumisha Muungano wa Tanzania na kuepuka viashiria vyote vinavyoonekana kuvunja muungano, hivyo tushikamane katika kuudumisha”. Alisema Ndugai.

Naye Mjumbe wa Bunge hilo ambaye mjumbe wa secretariati ya marekebisho kanuni za Bunge Maalum Mhesh. Evod Mmanda alisema kwamba miaka 50 ya muungano ni faraja na jambo la kujivunia.

“hatuna budi kwa pamoja kukaa na kuufikiria zaidi Muungano na kutatua changamoto zote zinazojitokeza ili kuudumisha muungano huu na Wasiopenda Muungano  hawana sababu za kutosha” Alisema Mh. Mmanda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. sio kweli ndugu jobu , ingelikuwa ni jambo la kujivunia na la mafanikio tungeona nchi nyengine kuiga mfano wetu , lakini katika kipindi cha miaka hamsini iliopita tumeona mataifa mbalimbali yakimeguka , kama sudani kusini , eritrea , timori mashariki , urusi , chekoslovakia , kosovo ,yugoslavia na mengineyo mengi ambayo yako njiani kujitenga kama scotland, tusidanganye wananchi bure tuwe wakweli na waadilifu , msema kweli mpenzi wa mungu

    ReplyDelete
  2. Maoni yako na tunayaheshimu ila tuachiwe tupumue

    ReplyDelete
  3. waachieni wazanzibari kama hawataki tumekuwa tukiwalazimisha kitu hawataki miaka yote , umefika wakati tukubali ukweli huu muungano hautakiwi kule visiwani basi tuwaache, bado tumeungana kwenye mambo mengine kama kuchanganya damu nk kwa hio uhusiano wetu utabakia pale pale, wengi wape na hio ndio maana ya demokrasia, ndugu zetu wa visiwani wameshaonyesha kuwa wengi wao hawautaki muungano na sisi kiserikali, na sisi baadhi ya watanganyika tunahisi tutakuwa na uhusiano bora na zanzibar tukivunja muungano , kama mke na mume waliopeana talaka na kuishi kwa amani , kuliko kuishi na ndoa yenye matatizo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...