Watanzania Wameshauriwa Kuwekeza kwenye Mifuko Iliyo Chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Kwa Lengo la Kuwekeza kwaajili ya Maisha mara Baada ya Kusataafu.

Wito Huo Umetolewa  na Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano Kutoka Dhamana ya uwekezaji Tanzania Bwana Daudi Mbaga Wakati Akitoa Mada Kwenye Semina ya wafanyakazi Wanaokaribia Kustafu Inayoendelea Mkoani Morogoro.

Alisema Kwamba Watanzania Wengi huwa hawajui Nini Cha Kufanya Pindi Wanapostaafu Hali Inayosababisha Watanzania Wanapostaafu wakishapokea Mafao Yao wanajaribu Kufanya Kila Shuguli Mbalimbali Lakini Kutokana na kutokuwa na Uzoefu wa Shuguli Hizo shuguli  nyingi hazidumu.

Bw Mbaga Amewashauri Watanzania  hasa Wale wafanyakazi wanaokaribia Kustaafu Kuwekeza  Mifuko iliyopo Chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Kama MFUKO WA JIKIMU Wenye "Kauli Mbiu Ishi Vizuri Unastahili". Kwa Lengo la Kuwasaidia Wastaafu Ili Kuondokana na Kupata Hasara na Kufurahia Maisha Zaidi Mara Baada ya Kustaafu.

Ameongeza Ni vizuri kwa watanzania kuwekeza katika Mfuko Huo kwa kuwa Upo Chini ya taasisi ya Serikali  na uwekezaji wao ni wa Uhakika.Pia Kuwekeza Katika Mfuko Huu watanzania watapata Faida Nyingi kwani Mfuko Huu Unaendeshwa Kitaalamu na Wataalamu Waliobobea Katika Msawala ya Uwekezaji ,Urahisi wa  wawekezaji wanaweza kufuatilia Maendeleo ya Masoko ya FedhaKwa Kufuatilia Mandeleo ya Mifuko.

Mkurugenzi alisema Uwekezaji katika Mfuko Huo ni wa Uhakika kwasababu Unampa Mwekezaji Unafu wa Gharama za Uwekezaji, Uwazi ,Faida Nzuri,Urahisi wa Kujiunga katika Mfuko Huu.
Mkurugenzi wa Masoko Na Mahusiano Kutoka  Dhamana ya Uwekezaji  Tanzania Bwana Daudi Mbaga Akitoa Mada Kuhusu Kuwekeza kwenye Mifuko Iliyo chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Kwajili ya Maisha Mara Baada ya Kustaafu kwenye Semina ya Wafanyakazi wanaokaribia Kustaafu Iliyoandaliwa na TAGLA Mkoani Morogoro.
Washiriki wa Semina ya Wanaokaribia Kustaafu Wakifuatilia Kwa Makini Mada Iliyokuwa Ikitolewa Kuhusu Uwekezaji katika Mfuko wa Jikimu Iliyokuwa Inatolewa Na Mkurugenzi wa Masoko  Ndugu Daudi mBAGA (hayupo Pichani)Kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Inayoendelea Mkoani Morogoro
Mkurugenzi Mwandamizi wa Masoko na Mahusiano Kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Bi Martha Mashiku Akieleza Faida za Kuwekeza Katika Mifuko iliyo chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania.Bi Martha Liwashauri Watanzania Kjiunga katiaka Mifuko Umoja Fund,Wekeza Maisha,Mfuko wa Watoto,Mfuko wa Jikimu,Na Ukwasi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Suala la Uwekaji Akiba ya Kifedha kwa Mtanzania bado uelewa upo chini sana.

    Wengi wa Watanzania wa kaiwaida wanafikiri kitu kama kufungua Akaunti ya Benki ana kuweka Akiba ni mpaka umiliki Mamilioni ya Shilingi!

    Kitu ambacho siyo kweli, kwa kuwa Kikanuni kila Kipato upatacho hata kama ni Tsh. 100/- kwa siku ni lazima pawepona sehemu yake utatumia na sehemu utaweka akiba.

    Yaani chukua tumia 80% ya Tsh.100/- (ambayo ni sawa na Tsh.80/-) huku ukiweka akiba ya 20% ya Kipato hicho yaani Tsh. 20/-)

    Hivyo kwa Mtazamoutaona ni ndogo lakini ukipiga hesabu kwa mwaka hadi miaka zinakuwa ni Fedha nyingi sana!

    Mfano kwa mwaka:

    Akiba 20/- Tsh. X 360 = Tsh. 7,200/-

    FEDHA AMBAYO HAKUNA SACCOS AMA BENKI ITAKUPATIA BURE LABDA MWISHONI MWA MWAKA KWENYE KRISMASI UKUTANE NA FATHER KRISMASI NDIO UTAIPATA BWERERE BWERERE!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...