Watanzania Wisconsin wamezuia kuchomwa moto kwa mpendwa wetu Michael Lukindo aliyefariki Jumapili ya March 16, 2014 wameomba msaada kwa Watanzania wengine waishio Marekani na kokote pale Duniani kujitahidi kadri tuwezavyo tuweze kumstiri Mtanzania mwenzetu ghrama za mazishi ni $6,000 
jina la AC ni Memorial for late Mike Lukindo 
Benki ni Madison Chase Bank AC ni 579362299 
Route ni 075000019 
Tafadhali ndugu zangu, Watanzania wenzangu msiba huu ni wetu sote chochote utakachokua nacho kitasaidia kumzika ndungu yetu asante

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Sasa kama marehemu mwenyewe aliamua kabla hajafariki ya kwamba atakuwa cremated akitangulia kwenye haki, na kama mkewe na watoto wamekubaliana nae, ninyi wengine yanawahusu kivipi? kwani hata cremation pia ina gharama zake.

    ReplyDelete
  2. MsemaKweliMarch 30, 2014

    mmh hawa Watanzia wa Madison, WI wana matatizo gani? Mtu na familia yake wamekubaliana kuwa akifariki awe "cremated". Hayo ni mazishi kama kumfukia mtu kwenye udongo, iweje leo wao wala sio ndugu waanze kuingilia mambo ya familia hii? Huyu kwanza mmeambiwa ni African American maana yake alishakuwa raia wa Marekani na sio Mtanzania kama mnavyotaka iwe. Acheni kuingilia mambo ya kifamilia.
    MsemaKweli.

    ReplyDelete
  3. That is just the body. the real john is in heave with jesus. the body is like the house or the jacket which enables us to live on this earth. once simeone dies it does not matter whether one is cremeted or buried.
    Just have peace with you guys.

    ReplyDelete
  4. Diaspora bwana! Sasa mambo ya Kifamilia mnaingilia nini?

    Ikiwa Mume ambaye ni marehemu walikubaliana na mkewe mazishi yawe ya kuchoma mwili kwa moto, nyie diaspora ya Ki-Tanzania inawahusu nini?

    Sana sana ni uiletea uchungu familia ya marehemeu yaani Mkewe na wanae.

    Mdau
    Kijitonyama

    ReplyDelete
  5. Jackson went to heaven and see john in heaven with jesus....and who is in hell with sheitani jackson??......mdau hapo juu msema kweli....kuchukua uraia wa marekani hau change your ethnic group aliposema african amerikani alimaanisha mke wake ndio africanamerican.....

    ReplyDelete
  6. Those who have decided otherwise, should put 6000 down and finish the job. Aliewaambia watanzania ni wa kuomba omba ni nani?

    ReplyDelete
  7. Diaspora mnataka manataka uraia wa nchi mbili mje kuwekeza!! $6000 nazo ni za kuchangishana kwenu!!kuanza kuomba michango!!

    ReplyDelete
  8. Hao wafuasi wa John Mashaka wanakazi kweli .itabidi waheshimu familiar us marehemu

    ReplyDelete
  9. Kwanza mna uhakika gani huyo ni Mtanzania kweli? Passport za Tanzania zinatumiwa na watu wengi tu wa mataifa mengi, so inawezekana wala sio mbongo.

    Pili, kama hata kama ni mtanzania familia yake na mwenyewe alishaamua achomwe moto sasa hicho mnachofanya ni kuingilia mambo ya familia, inawezekana alijua alidanganya hata uraia ndio maana hakutaka ajulikane mkianza mambo ya kutaka kusafirisha mwili. Hata kama uko nje sio sababu ya kuachana na familia yako, sie pia tuna ndugu wako nje na wanawasiliana nasi kila wakati kujua kinachoendelea home. So, huyo sio mtanzania.

    Tatu, mbona watanzania tulioko bongo tunapata na matatizo na wala nyie wana diaspora hatuoni michango yenu? Kama mmeamua kujitwisha mzigo usio wenu bebeni wenyewe.

    Nne, wale waliokwenda huko nje wakasahao kama wana ndugu tz na mkshaoa hao sijui black America mkipata matatizo msitutafute. Msijisahau jamani kumbukueni mliowaacha home huo ndio undugu sio wa kutafutana kwenye matatizo.

    ReplyDelete
  10. Kama watanzania wote mlioko huko mnakosa dola 6000 basi rudini tu huku, huku tunazika hata hatuwaambii gharama fuateni maagizo ya marehemu hakutaka mwili wake usumbuliwe wala kuwasababishia usumbufu watu wengine...

    ReplyDelete
  11. It is beyond me why all of a sudden the death is transferred from a family matter into a communal issue. In looking fir family members, the widow may only have sought to get them informed and surely not to trigger a debate of whether or not the body should be cremated. Moreover, a debate among non-relatives!

    ReplyDelete
  12. Wabongo tuna mdomo sana, jamaa kelele mpaka kilioni. Naona siku hizi maadili ya kuheshimu shida za wenzetu hamna, ili mradi tufanikishe mawazo yetu. Uzuri wa mauti yanatukuta wote, uwe Bongo au popote pale shida ipo. Vile vile watu wanaongea kwa dharau sana siku hizi kana kwamba wenyewe ndiyo matajiri sana, mfano hao wanaosema hawaa jamaa wanachangisha $6000, mala sijui wanajifanya wawekezaji. Wacheni kelele za mitandaoni jamani, mtu kutoa hata shillingi moja ni moyo wake mwenyewe. Hela haziokotwi Ughaibuni.Mwekezaji anapowekeza ana amini atapata faida fulani. Wawekezaji wageni wanapowekeza tunaona kabisa wanapeleka wapi faida zao,(mfano madini). Na uhakika wabongo wengi wanapowekeza kwao wanasadia faida kubaki Bongo, jamii kifikra, na maendeleo. Pia utaifa unatumaliza kwani ulimwengu unasonga mbele. Tumeona mifano mibaya ya utaifa kama Hitler, Watusi na Walundi. Na sasa tunasema Wanzizabari siyo ndugu zetu, hapo tutaanza kusema tugawane kimakabila na kidini badala ya kuongelea umoja. Tunaelekea pabaya.
    Amkeni wabongo!!!

    ReplyDelete

  13. Tunasikitika sana na kifo cha mwenzetu Mike Lukendo Madison, ambaye ni Mtanzania. Mike alionyesha ufahari na mafano mzuri kwa wegine kwa kupanga mwisho wamaisha yake na kukubaliana na familia yake. Kwa kawida yetu sisi watanzania tunaishi huku ugaibuni, tuko karibu sana kama ndugu na kwa haya mambo ya vifo tuna watu ambao ni karibu na familia ya mfiwa-kwa mfano mke wake, mtoto wake au kiongozi wa Community. Habiri hii haina simu wala jina la mtu a ambaye anahusiaana na marehemu isipokuwa benki account. Lazima tuwe na makini kwa sababu dunia ya leo in wajanja wengi. Huyo mwombaji au waombaji mchango watoe majina yao, simu simu zao, na picha zao

    Temba
    Deputy Treasurer
    NEW YORK TANZANIA COMMUNITY
    https://www.facebook.com/pages/New-York-Tanzanian-Community-Inc/166418816757062

    ReplyDelete
  14. Hamna atakayetoa mchango miaka yote hiyo alokaa hana hata pesa kwenye account yake that shame family yake pia hawana pesa za kumzika simple mchomeni moto tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...