Mpango wa Taifa wa Damu salama kwa kushirikiana na waumini wa dhehebu la Sabato wameendesha zoezi la kuchangia damu katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Mikoa hiyo ni Dar-es-salaam, Dodoma, Mwanza, Kilimanjaro,Tabora, Mara, Morogoro, Mbeya na Iringa, lengo likiwa  ni kukusanya chupa 3000 katika mikoa hiyo.
Akiongea na waumini waliofika katika kituo cha Damu salama ilala mchikichini Askofu wa Jimbo la Mashariki ambalo linajumuisha mikoa ya Dar-es-salaam, pwani, Dodoma, Morogoro, Lindi, Mtwara na Zanzibar Askofu Mark Walwa Malekana aliwashukuru waumini kwa moyo wa upendo wa kuja kuchangia damu.
Amewaomba waendelee na moyo huo ili wawe wachangia damu k wakujirudia kwani amesema mwanaume anaweza kuchangia mpaka mara nne kwa mwaka na mwanamke mara tatu kwa mwaka . 
Askofu Mark Walwa Malekana pia alikemea tabia ya baadhi ya watumishi wa hospitali ambao wanajihusisha na tabia ya kuuza damu kuwa waache tabia hiyo kwani ni dhambi.
"Watu wanajitolea kwa hiari na upendo kuchangia damu bila malipo yoyote hivyo wanapaswa kupata huduma hiyo bure", aliasa Askofu Malekana.
 Askofu Mark Walwa Malekana akiongea na waandishi wa habari ambao walifika ilala mchikichini kushuhudia waumini wakichangia damu.
 Afisa mwendeshaji Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dr. Abdu Juma akimshukuru Askofu Mark walwa Malekana kwa kuhamasisha waumini wa makanisa ya sabato kujitolea damu kwa hiari kuokoa maisha ya wagonjwa
 Meneja wa Damu salama  kanda ya Mashariki Dr. Avelina Mgasa akimkaribisha askofu kuongea na waumini
Zoezi la kuchangia damu likiendelea jijini Dar es salaaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...