Mnamo tarehe 27.03.2014 majira ya saa 02:10 usiku huko Gulwe katika Wilaya ya Mpwapwa kulitokea ajali ya treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Kigoma baada ya kusombwa na mkondo wa maji ya mvua zinazoendelea kunyesha. Kutokana na wingi na nguvu ya maji hayo ilifanya kichwa cha treni hiyo kutumbukia kwenye mto Mimo.

                VIFO:
Ajali hiyo hadi hivi sasa imesababisha vifo vya watu wawili ambao wamefahamika kwa majina yafuatayo:-
1.  Felix s/o Kalonga
2.  Ismail @ Suma

              MAJERUHI:
        Waliojeruhiwa ni kama ifuatavyo:-
1.   Hassan s/o Kitambo, Miaka 89, Mkazi wa Kidete – Amelazwa katika Hospitali ya Mpwapwa.

2.   Reuben Ngasongwa, Miaka 43 – Amehamishwa kutoka Hospitali ya Wilaya Mpwapwa kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

3.   Michael Lupatu, Miaka 52 – Amehamishwa kutoka Hospitali ya Mpwapwa kwenda Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
  
4.   Ramadhan Kanenda, Miaka 34,  – Amelazwa Mpwapwa Hospitali.

5.   Mohamed Salum, Miaka 25,  - Alitibiwa na kuruhusiwa

6.   E.2699 CPL Mfaume – Ametibiwa na kuruhusiwa.

7.   E.3295 CPL Respis – Bado amelazwa Mpwapwa Hospitali.

Bado jitihada za kuwatafuta watu wengine wanne ambao hawajulikani walipo zinaendela.

Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Poleni kwa maafa ya ajali.

    Sasa tumepewa majina ya walio kufa wa2, majeruhi 7 je hao wa4 wasio julikana walipo wajina yao ni yapi?

    Kwa kawaida wahanga wa maafa huweza kupaa mtikisiko wa Kisaikolojia kwa kushikwa na bumbuwazi, kuwa kama mataahira ama mabubu wa muda, wakafika sehemu tulizopo na wakabaki kimya wasiseme walikotokea ama wao walikuwepo kwenye eneo la ajali.

    Inawezekana tukahangaika kuwatafuta huko Gulwe-Mpwapwa, Dodoma kumbe kwa kiwewe wakajikuta wanatimua mbio vichakani msitu kwa msitu na kufika hadi Morogoro ama Chalinze kwenye mpaka wa mwisho wa uzee!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...