Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiongea wakati alipofungua mkutano  mkuu wa mwaka wa chama cha viziwi mkoa wa Ruvuma (CHAVITA) leo katika ukumbi wa Maktaba ya mkoa.Kushoto ni mwalimu Rehema Nyagawa ambaye ni mkalimani wa kujitolea.
Grevas Komba na Bahati Nyoni ambaye ni Katibu wa Viziwi mkoa wa Ruvuma wakisoma risala ya viziwi kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiwa katika picha ya pamoja na wananchama wa Chama cha Viziwi Mkoa wa Ruvuma mara baada ya kufungua mkutano wa mwaka wa chama hicho hivi leo mjini Songea.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Thabit Mwambungu amewataka wazazi wenye watoto walemavu wakusikia (Viziwi) kutowaficha ndani badala yake  watoe taarifa kwa viongozi wa serikali za vijiji na mitaa ili wasaidiwe kupatiwa huduma muhimu ya elimu.

Ametoa wito huo leo wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha Viziwi mkoa wa Ruvuma (CHAVITA) ambapo amewahakikishia kuwa serikali inathamini na kuwatambua viziwi kuwa ni kundi maalum katika jamii linalohitaji elimu maalum

Ameongeza kusema kuwa huduma zote anazo hitaji binadamu pia zinahitajiwa na watu wenye ulemavu wa kusikia nakusema kwani hayakuwa matash iyao kutaka ulemavu huo.

“Ulemavu wa kutokusikia au kutokuzungumza si laana kwani tatizo hili linaweza kumpata mtu yeyote yule” alisema Mwambungu

Amewasihi wazazi na walezi wote mkoani Ruvuma kuwapeleka shule watoto viziwi kwani elimu husika kwa wasio sikia au kuzungumza ipo na inatolewa bure katika shule maalum za umma.

Ameitaja shule maalum kwa viziwi ya Ruhuwiko iliyopo Songea Manispaa kama mfano wa shule zinazotoa elimu kwa watoto wasio sikia na kuzungumza hivyo ni vema sasa wananchi wakawapeleka watoto kupata ujuzi na maarifa ya takayo wasaidia kujikimu na maisha.

Mwambungu ameziagiza halmashauri zote mkoani Ruvuma kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa walimu wenye taaluma za kufundisha watu wenye ulemavu ili kusaidia kufundisha katika shule zenye watoto viziwi au wasioona ili walemavu hawa wapate mawasiliano stahiki.

Katika kusaidia jitihada za CHAVITA kujitangaza na kuunda umoja wao Mkuu wa Mkoa,Mh. Mwambungu amewachangia shilingi laki nne (400,000/=) ili kutunisha mfuko wa viziwi mkoa wa Ruvuma na kuwasihi watu wenye mapenzi mema kuwasaidia walemavu wa aina zote.

Katika risala ya CHAVITA kwa mgeni rasmi iliyosomwa na Grevas Komba wameomba suala la elimu lipewe kipaumbele kwa viziwi kwani hakuna vituo vya kutosha kwa mafunzo kwa viziwi.

Pia wameomba serikali kudhamini walimu watakao saidia kutatua tatizo la wasio sikia ili wapate wakalimani wenye ujuzi na utaalam wa mawasiliano.

Mkoa wa Ruvuma kwa mujibu wa takwimu za CHAVITA unao viziwi 256 walio tambulika kwa wilaya zote tano ambapo wengine hawajahesabiwa kutokana na kufichwa na wazazi na walezi wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...