Mwenyekiti wa Bongo Movie, Bw Steve Nyerere akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa East 24 uliopo Arcade house Mikocheni.
 Steve Nyerere akinadi kinywaji cha Windhoek ambao ndio wadhamini wakuu wa sherehe ya Kutimiza Miaka 3 ya kuzaliwa kwa Bongo Movies, Sherehe itakayofanyika katika Ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House Mikocheni jijini Dar Es Salaam Ijumaa ya tarehe 28.
Rais wa FM Academia Nyoshi Ali Sadat akiongea na wadau waliofika katika ukumbi wa East 24 wakati wa utambulisho wa wasanii na bendi zitakazotoa Burudani siku ya Sherehe ya Kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie itakayofanyika katika ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House ijumaa ya tarehe 28 Mwezi huu
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Mabibo Beer, Bw Jerome Rugemalila akiongea na Waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa Bendi na wasanii watakaotoa burudani ya nguvu siku ya sherehe ya Kuzaliwa kwa Bongo Movie itakayofanyika tarehe 28 katika Ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House Mikocheni Jijini Dar.
 Baadhi ya wasaniii wa Bongo Movies wakifuatilia kwa makini 
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer, Benadetha Rugemalira (aliyeshika kinywaji cha Climax) akifuatilia kwa makini matukio wakati wa utambulisho wa Wasanii na bendi zitakazotoa burudani siku ya ijumaa kwenye sherehe ya Kuazimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa Bongo Movie
 Baadhi ya wadau waliohudhuria utambulisho huo uliofanyika katika ukumbi  wa East 24
 Mkurugenzi Mkuu wa Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalira (kulia) akijadiliana jambo na Meneja masoko wa Mabibo Beer, Jerome Rugemalira (pili kulia) na Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Bwa Steve Nyerere na Msanii wa bongo movie Adam Kuambiana
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere akijadiliana jambo na Katibu wa Bongo Movie Mtitu wakati wa utambulisho wa Wasanii na bendi zitakazotoa burudani wakati wa sherehe za kutimiza miaka mitatu ya kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...