Baadhi ya shule za msingi na sekondari katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, zikiongoza maandamano ya wananchi kuhamasisha kulinda na kuhifadhi maliasili za nchi katika kuadhimisha siku ya wanyamapori duniani, tarehe 3 Machi 2014.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru, Bakari Chande Nalicho (wa kwanza kulia), wawakilishi wa WWF-Tanzania Rodney Ngalamba na Nalimi Madata, mkurugenzi halmashauri wilaya ya Tunduru John Kamwela na afisa maliasili wilaya ya Tunduru Japhet Mnyagala, wakipokea maandamano ya wananchi katika kuadhimisha siku ya wanyamapori duniani, mjini Tunduru, mkoani Ruvuma.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru, Bw. Bakari Chande Nalicho, akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo (hawapo pichani) juu ya utunzaji na uhifadhi maliasili ikiwemo wanyama pori kama tembo, katika maadhimisho ya siku ya wanyamapori duniani tarehe 3 Machi, 2014.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru, Bw. Bakari Chande Nalicho, akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo (hawapo pichani) juu ya utunzaji na uhifadhi maliasili ikiwemo wanyama pori kama tembo, katika maadhimisho ya siku ya wanyamapori duniani tarehe 3 Machi, 2014.
Baadhi ya wananchi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya hiyo (hayupo pichani), Bw. Bakari Chande Nalicho,alipokuwa akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya wanyamapori duniani, taehe 3 Machi, 2014.
Kikundi cha uchumi na sanaa Mkanyageni – KIUM, kikitoa burudani katika mkutano wa wananchi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma katika maadhimisho ya siku ya wanyamapori duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...