Ankal salamaaaa?
Leo katika pita pita zangu,nilibahatika kupita Barabara ya Nyerere mbele ya Mataa ya Tazara,nililikuta Gari hili lililazimishwa kugeuzwa katika sehemu ambayo si salama na wala hairuhusu kufanyika hivyo,kwani pia gari hilo lilikuwa linakanyaga sehemu ya baraza la kati lilalotenganisha upande mmoja na mwingine wa barabara.
Nilimshangazwa sana na yule Jamaa ambaye inaonekana dhahiri kuwa aliona uvivu au ugumu wa kwenda kwenye kona inayomhusu ili akate kulia na ageuze Lori lake hilo.
Nilikasirishwa sana na kitendo hicho na ilinitia uchungu sana kuona kodi zetu zinaharibiwa kizembe hivi,nikasisimama na kuanza kumueleza Dereva huyo ambaye alianza kupayuka kwa nguvu na kama kawaida mimi ndie nilieonekana mjinga kwa wapita njia maana wao hawakujali.
Naomba Wahusika wamsake muharibifu huyu wa miondombinu yetu ili kina Dkt Magufuli na Tanroads wamshughulikie.
Mdau Mpenda Maendeleo ya Nchi.
Sehemu ya Uharibifu uliofanywa na Dereva huyo.
Next time chukua namba ya gari ili dereva na mwenye gari waje wajenge hapo walipomoboa...sijuhi ni lini tutastaharabika....
ReplyDeleteHuu ndiyo uzalendo, lakini mbona mdau umeshindwa hata kupiga picha sehemu ya mbele tuweze kuona plate namba? Hapo kwa kweli umechemsha na ndiyo maana hata watu walikuona weye ndo mwenye matatizo...gari hutambulika kwa Registration Number yake na siyo maandishi ya ubavuni. Leta namba yake ashughulikiwe
ReplyDeleteNdio tatizo letu wengi wabongo. Tunafikiria sasa tu, hatujali wengine wala kesho. Unaona tunavyoharibu taa za barabarani? Reli zinavyoibwa? Kweli hata iwepo gesi ya wapi tutaendelea kweli?
ReplyDeleteKuna haja ya kutoa elimu kama ya darasa la kwanza. Watanzania wengi wanajidai kutafuta maendeleo lakini wanaharibu uchumi. Mpiga picha umefanya vema kabisa. Ila siku nyingine piga plate number. Shame on you driver of the lory. Mkiambiwa punguzeni uzito mnakuja juu, barabara zetu mnaziharibu hata hapo. Kana kwamba ninyi ndo mnalipa kodi peke yenu. Acheni ujima. Jengeni nchi yenu.
ReplyDeleteingawa ni kosa la dereva , lakini uendeshaji wa magari makubwa inatakiwa ujuzi , lakini vile vile msisahau hichi kibaraza hakikujengwa kwa kwa kiwango kinachotakiwa , kawaida kama kimejengwa vizuri kwa mchanganyiko sawa , huwa hakimon'gonyoki kikipandiwa na gari hata liwe zito vipi ,
ReplyDeleteThe mdudu,madeleva kama hao huwa sio watanzania so they dont care na kama ni mtanzania ni mwehu wa akili au ni jilevi la mchana kweupe,dawa ya hao madeleva ni kujichukulia shelia mkononi achomwe moto au hilo lori lake ndio liteketezwe kwa moto,nawashangaa watanzania walivyo wajinga hapo angekua mkwapua simu tayari wangeshamchoma moto,amkeni watanzania wachomeni moto wajinga kama hao coz kama ni umauti amejitakia mwenyewe.hayo ndio anayokemea MWANAMZIKI WA UKWELI AFANDE SELE KWENYE HIYO SINGLE YAKE MPYA YA MWENDO KASI.
ReplyDelete