Bw. Sultan A. Sultan akitoa mada wakati wa kongamano la viongozi lililojadili mada kuu isemayo ‘Rasilimali za Taifa kwa amani na Maendeleo, Bagamoyo , Pwani tarehe 20 Machi,2014.
===== ====== =====
Zipo fursa nyingi kwenye uchumi wa gesi- Sultan
Na Malik Munisi, Bagamoyo.
Watanzania wameaswa kutambua fursa zitokanazo na rasilimali zinazogunduliwa nchini ili waweze kunufaika kutokana na uwepo wa rasilimali hizo.
Hayo yamebainishwa na Bwana Sultan Sultani mkazi wa kilwa alipokuwa akitoa mada juu ya ‘‘Ushiriki wa wenyeji katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia’’, katika Kongamano la Viongozi lililojadili mada kuhusu “Rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania” lililofanyika Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Bw. Sultani alieleza kuwa, wananchi wanatakiwa kuelewa fursa mbadala zipatikanazo kutokana na uwepo wa rasilimali za gesi na mafuta nchini zikiwemo ununuzi wa hisa kwa makampuni makubwa ili kuwawezesha kuongeza mtaji yao ambapo faida yake itapatikana mara tu baada ya gesi kuanza kuuzwa.
Aidha, alitaja fursa nyingine kuwa ni uwezekano wa uhitaji mkubwa wa majengo na maghala yatakayohitajika kwa ajili ya kutunza vifaa na pembejeo muhimu kwa ajili ya utafutaji na uzalishaji wa gesi katika maeneo yaliyoko baharini.
Alizitaja fursa nyingine kuwa ni pamoja na makampuni ya ulinzi, kampuni za usafirishaji, maabara, vyuo maalumu vya kuelimisha umma katika tasnia ya petroli na nyanja zake, makampuni ya kutunza mazingira, usalama na afya, na kuongeza kuwa hizo ni baadhi tu ya fursa zitokanazo na uwepo wa rasilimali gesi na mafuta nchini.
Pamoja na hayo, alieleza uwekezaji katika mafuta na gesi si bahati nasibu ya kutoa moja ukapata milioni moja bali ni ile ya kutoa mamilioni kama sio mabilioni na kisha ukaambulia patupu. Hivyo, alisisitiza kuwa, mifano ipo ya watu walionunua leseni za utafiti kwa kuwekeza mabilioni wakaishaia kukosa na matokeo yake wakapoteza maisha kwa maradhi ya moyo au msongo wa mawazo.
“Pamoja na kuwa sayansi ya hali ya juu kutumika katika utafiti wa mafuta na gesi, bado kwa kiasi kikubwa ugunduzi wa rasilimali hizi ni wa pata potea huku uwekezaji wake ukiwa ni wa ghali sana” aliongeza Sultan.
Alisisitiza kuwa, yapo makampuni mbalimbali yaliyofika nchini ili kuwekeza katika maeneo ya Songosongo (Lindi) na Msimbati (Mtwara) ambapo mengi yaliingia kwa kifua mbele lakini yakatokea kwa mlango wa nyuma kutokana na ugumu wa kazi hiyo na kufanya utafiti bila ya mafanikio.
Mwisho Sultan alihimiza umuhimu wa wananchi kuelezwa mapema ugumu na pata potea iliyopo katika sekta ya mafuta na gesi ili wananchi waweze kuzitambua fursa na kujihusisha katika kuanzisha biashara katika maeneo mbalimbali ili waweze kutoa huduma kwa wawekezaji wanaofanya utafiti na wale wanaoendelea na shughuli za uchimbaji wa gesi asilia, ikiwemo elimu ya soko la hisa ili iweze kuwasaidia wananchi kuwekeza katika makampuni ya mafuta katika namna ambayo itawanufaisha.
Kasema Kweli Sultan hakuna hisia za watu zinazoathirika hapo. Mimi nimefanya kazi katika hii sekta kwa muda wa miaka 20. Pata potea na hata kukosea katika ustafiti huweza kusababisha upotefu wa mambilioni ya hela za mjasiria mali.
ReplyDeleteIsitoshe gharama ni kubwa mno za utafiti na uchimbaji kisima kimoja tu, kwa mfano:
Gharama za (utafiti kwa mtetemeko) 3 D Seismis kwa kitalu kama eneo la mkoa wa pwani inakaribia Usd 150m
Gharama za kukodi rigi la utafiti ni kuanzia usd 500k-3m inategemea ni rig aina ya rig na hiyo ni nchi kavu.
Drilling pipes za kisima chenye kina kama 5000mts zinaweza kufikia 12m usd
Well head and accessories zake kama BOP valves 1.2m.
Hapo hatujaweka overheads kama Mishahara ya Drilling Engineer na Tool Pusher mbali Bima ambayo ni kali sana. Huyo Driller bima yake ya maisha tu onaweza kufikia 1m usd. Huyo Pusher mshahara wake si chini ya Usd 20 alfu. Bado drilling mud ambayo ni ghali sana. Bado Drill bits amabazo inategemea na formatio kule chini kama kuna mwamba ndio unaweza kutumia drill bits nyingi na drill bit ya rahisi si chini ya dola 15000.
Bado drilling camp pamoja na huduma zake.
Logistic cost nazo.
Msikae kuonta tu wazawa tupewe vitalu. Usidhani ni gharama za kuchimba visima vya maji Mkuranga.
Halafu