Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akionyesha simu ya Aina ya Samsung S5 mara baada ya kuzindua ofa itakayowawezesha wateja wake kununua simu hityo na kujipatia vifurushi vya muda wa maongezi, sms pamoja na data bure.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza ofa kabambe inayowawezesha wateja wake kununua simu ya kisasa ya aina Samsung S5 na kupata vifurushi vya muda wa maongezi, sms pamoja na data bure.

Akiongea wakati wa kutangaza ofa hiyo Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema” leo tunayofuraha kuwatangazia wateja wetu ofa kabambe ambayo inawawezesha kununua simu ya Samsung S5 na kupata dakika 1500 bure , SMS 5000 kutuma mitandao yote pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB kitakachomwenzesha wateja wetu kuperuzi katika mitandao kama vile facebook na twitter kupitia huduma yetu ya internet ya 3.75G yenye kasi zaidi. 

Vifurushi hizi vitadumu kwa muda wa mwenzi mmoja kuanzia tarehe ambayo mteja atafanya manunuzi ya simu ya Samsaung S5”.

Simu hii ya Samsung S5 inapatikana katika maduka ya Airtel yaliyopo Moroco, Mlimanicity, Jmall pamoja na maduka yote ya Samsung pamoja na maduka yanayouza simu za smart phones yaliyoko nchi nzima.

Tunachukua nafasi hii kuwahimiza watanzania kuwa wakwanza kuchangamkia ofa hii” aliongeza Jane Matinde

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mbona bei hamjataja.....?

    ReplyDelete
  2. Sasa mbona hakuna bei au offa ni ya bure?

    ReplyDelete
  3. Kuna kasumba nimeisoma hapa Tz...yani kuweka bei ya kitu ni dhambi...pleni kwa hilo...nimekuwa put off baada ya kuperuzi kama kuna bei na kuambulia tarakimu za sijuhi GB sijuhi nini...kwaherini....

    Mjifunze marketing; buyers hawana muda....yani ninyanyue mguu wangu hadi duakni afu nikutane na bei ambayo sina uwezo nayo...hell no!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...