Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi limekutana Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Eng. Alhaj Mussa Iyombe ambaye pia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo ambaye wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo, Eng. Iyombe aliwajulisha wajumbe waliohudhuria kikao hicho kuwa, madhumuni makubwa ya kuwepo kwa mabaraza ya aina hii ni kushirikisha wafanyakazi katika utekelezaji wa shughuli za wizara ikiwa ni pamoja na kuwaweka wafanyakazi hao karibu na uongozi wao.
Baraza hilo ambalo linaundwa na wajumbe kutoka katika taasisi zote zinazosimamiwa na Wizara ya Ujenzi, ndilo pia chombo cha kutoa ushauri kwa uongozi na ufuatiliaji wake hasa kwa masuala yanayohusu maslahi ya wafanyakazi.
Alisema kuwa Baraza hilo ndilo vile vile chombo kinachotoa fursa kwa viongozi kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa wafanyakazi wanaowaongoza.
“Hapa tutatathmini pia upandishwaji vyeo kwa wafanyakazi pamoja na taratibu za mafunzo” alisisitiza Eng. Iyombe na kuongeza kuwa katika kikao hicho ajenda kuu itakuwa ni kupokea na kujadili mipango na makisio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha wa 2014/15.
Hata hivyo.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo aliwasilisha salamu za Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amelitaka Baraza hilo kujadili vile vile namna ya kuboresha mahusiano ya kati ya taasisi zinazosimamiwa na Wizara ya Ujenzi kwani kwa sasa mahusiano kati ya taasisi hizo si ya kuridhisha.
“Zipo huduma ambazo taasisi moja inaweza kupata kutoka taasisi nyingine iliyo chini ya wizara hii lakini inashangaza kuona huduma hizo zinatafutwa kutoka sehemu nyingine na tena kwa gharama kubwa” alihoji Waziri Magufuli.
Aidha, Waziri Magufuli amewataka watendaji wote kuwa na utayari wa kutekeleza majukumu yao wakati wowote wanapohitajika. “
Nyinyi watendaji mbali na utayari huo lakini pia ndio mnaotakiwa kusimamia mali za Serikali katika maeneo mnayoyasimamia” ilimalizia taarifa hiyo ya Waziri.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Alhaj Mussa Iyombe (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Samuel Mticco (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Joseph Nyamhanga (kulia).
Mkurugenzi wa Uatawala na Rasilimali watu Bi. Juliana Mwakitosi akichangia mada.
![]() |
Baadhi ya Wajumbe wakifuatilia mada |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Alhaj Mussa Iyombe (katikati waliokaa) akiwa na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kutoka katika Idara na Vitengo vya Wizara ya Ujenzi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Alhaj Mussa Iyombe (katikati waliokaa) akiwa na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kutoka katika Taasisi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...