Katika kilele cha kusherehekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Timu ya Zanzibar Heroes kupokea Jezi kutoa kwa wadhaminini wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ambazo jezi hizo zilitolewa na wageni rasmi waliohudhuria katika sherehe hizo akiwemo Mh. Mwigulu Nchemba ambae ni Mbunge na naibu waziri wa fedha na Uchumi Tanzania bara na upande wa Zanzibar pamoja na Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame mwakilishi na waziri wa nchi ofisi ya rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar. 
Naibu Mwakilishi Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa mataifa New York, Ramadhani Muombwa Mwinyi (kulia) akiwa pamoja na Viwe Juma, ambae ni Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya BENKI ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ambao ni wadhamin wa timu hiyo wakimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Zanzibar Heroes Abuu Qullatein Siku ya Jumamosi April 26, ndani ya Ubalozi wa Tanzania jiji Washington DC nchini Marekani, ili kujianda kupambana na timu ya Kilimanjaro Stars kwa mchezo wa kuwania Kombe la Muungano.
Viongozi: Wageni rasmi wa sherehe za Muungano Mhe: Mwigulu Nchemba (wapili kulia) akifuatiwa na Balozi Mulamula, pamoja na Balozi wa Waziri wa Nchi Zanzibar, Ofisi ya Rais na MBM Dr. Mwinyihaji Makame, (wakwanza kulia) Viwe Juma,wapili kulia ambae ni Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Zanzibar Heroes Abuu Qullatein katika Sherehe za Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Washington DC.

Wasimamizi wa timu ya Zanzibar Heroes Seif Ameir na Dedie Rouba wakionyesha jezi walizodhaminiwa na (PBZ) Benki ya Watu wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Viwe Juma akipata picha ya pamoja na Miss Tanzania USA
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Viwe Juma akipata picha ya pamoja na wanamitindo wa Mitindo Night.
Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Asociation Bwana Omari Ali akipata picha ya pamoja na mgeni ndani ya Ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Washington DC Nchini Marekani
Miss Tanzania USA akipata picha ya
pamoja na wanamitindo wa Mitindo Night
pamoja na wanamitindo wa Mitindo Night
Kawaida
Katika kilele cha kusherehekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Timu ya Zanzibar Heroes kupokea Jezi kutoa kwa wadhaminini wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ambazo jezi hizo zilitolewa na wageni rasmi waliohudhuria katika sherehe hizo akiwemo Mh. Mwigulu Nchemba ambae ni Mbunge na naibu waziri wa fedha na Uchumi Tanzania bara na upande wa Zanzibar pamoja na Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame mwakilishi na waziri wa nchi ofisi ya rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar.
Picha zote na swahilivilla.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...