Maelfu ya abiria waliotarajia kusafiri kwenda mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara walishindwa kufanya hivyo baada ya daraja la Mto Mzinga lililopo eneo la Kongowe, jijini Dar es Salaam, kubomoka na kusombwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Daraja hilo lilibomoka tarehe 13 Aprili, 2014 majira ya saa 12:00 asubuhi baada ya mabasi matatu kuvuka.

Daraja lilibomoka majira ya saa 12:00 na kufanya msururu wa mabasi yaendayo mikoa ya Kusini kushindwa kufanya safari zake na hata watembea kwa miguu hawakuweza kupita.

Kutokana na daraja hilo kubomoka, watu walioko upande wa Kongowe na Mbagala hawakuweza kuvuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Msururu wa mabasi ya abiria yanayofanya safari zake kwenda mikoa mikoa ya Lindi na Mtwara ulikuwa mkubwa , mabasi hayo yakiwa na abiria.

Tarehe 14.04.2014 saa nne na nusu usiku Dk.Magufuli alisimamia urudishwaji wa huduma hizo na watembea kwa miguu walianza kupita na kisha magari makubwa yalifuatia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...