Janneth Emmanuel
(kushoto), Cresenciah Herman (katikati) na Joshua Wambura
Stanslaus ambao ndio washindi wa Shindano la kusaka vipaji vya kuigiza Tanzania
lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa wanaonyesha zawadi zao za pesa
taslimu shilingi laki 5 kila mmoja mara baada ya kutangazwa washindi wa Kanda
ya Ziwa.
Shindano la Kusaka VIpaji vya Kuigiza Tanzania
lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents limemalizika leo kanda ya ziwa, Mkoani
Mwanza kwa washindi watatu kupatikana na kupewa zawadi zao. Washindi hao
ni Janneth Emmanuel , Cresenciah Herman na Joshua Wambura
Stanslaus huku binti mwenye umro mdogo kuliko washiriki wote Emiliana Fidelis
mwenye umri wa Miaka 11 aliweza kung'ara kwa kuonyesha kipaji cha hali ya juu
tokea mwanzo hadi Mwisho wa mashindano haya na kuweza kuvuta hisia za majaji na
kupelekea majaji kumtangaza mshindi wa shindano hili lakini kutokana na Umri
wake kuwa ni chini ya kigezo cha umri uliohitajika hatoweza kwenda Dar Es
Salaam Kwaajili ya fainali lakini majaji hawakumuacha bure walimpatia zawadi za
Shilingi laki Moja kama ishara ya yeye kuwa Mshindi pia.
Baada ya Mashindano haya kumalizika Kanda ya
Ziwa Mkoani Mwanza sasa Zoezi linahamia Kanda ya Kati Mkoani Dodoma wiki hii
ambapo Zoezi zima la usajili litafanyika kuanzi jumamosi ya tarehe 12 hadi 15
aprili ambapo pia watatafutwa washindi watatu pia wa kanda ya kati.
Washindi hawa watatu wataungana na washindi
wengine watakaopatikana katika kanda zingine katika fainali itakauofanyika
Mkoani Dar Es Salaam Na mshindi kupata Zawadi kubwa ya Shilingi Milioni 50 za
Kitanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...