Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo,katika mkutano wa hadhara,Kinana alijikuta akigeuka mbogo na kuwaomba radhi wakazi wa kata ya Kirema, Ikola na Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi, baada ya kubaini kuwa,kumekuwepo na kutowajibika kwa baadhi ya watendaji wa Serikali.Kinana amesema chama chake kamwe hakitowavumilia watendaji wanaoendekeza vitendo vya urasimu na umangimeza wa kutumia makaratasi ofisini badala ya kuwatumikia wananchi kwa kuwajibika ipasavyo.Kinana na Msafara wake wako mkoani Katavi kwa ziara ya siku nne ya kuimarisha uhai wa chama,kutekeleza na kuhimiza ilani ya uchaguzi ya chama hicho
Katibu
wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo.
Baadhi
ya Wananchi wa kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa
Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana alipozungumza nao kabla ya kukagua mradi
mkubwa wa soko la Samaki (Mwalo),ambao imeelezwa kuwa utapunguza
umaskini kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo. Hata hivyo
imeelezwa kuwa mradi huo wa soko na kuhifadhia samaki umechelewa
kukamilika na kupitisha miaka miwili ya zaidi ya muda ulipangwa kwenye
mkataba,Kinana amewahidi Wananchi kulifuatilia tatizo hilo na
kuhakikisha mradi huo unakamilika kama ilivyoahidiwa.
Mmoja
wa wakazi wa kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa
Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,akiuliza swali la zahanati na
,Elimu na Barabara kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana
(pichani kulia),alipozungumza nao kabla ya kukagua mradi mkubwa wa
Samaki (Mwalo).
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishirikii ujenzi wa mradi wa soko la samaki (Mwalo),katika kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,
Mbunge
wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso, akijibu na kutoa taarifa mbalimbali
kuhusiana na jimbo lake katika suala zima la kutekeleza na kuhumiza
Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010,mbele ya wakazi wa kijiji cha
Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...