Wateja wa Airtel wameipongeza kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia
bidhaa na huduma zake husisani huduma ya Airtel Money kuwa ni bora na
salama nchini
Huduma hii ijulikanayo kama "Hatoki Mtu Hapa" inawawezesha wateja wa Airtel
kutuma na kutoa pesa bila makato kwa kununua kifurushi cha wiki au cha
mwenzi cha Bure Pack na pia kuwawezesha wateja kutuma pesa kwa nusu
gharama ukilinganisha na ziwango vinavyotozwa sokoni. Ambapo kwa sasa
Airtel ndio kampuni inayotoza viwango vya chini vya miamala ya pesa nchini.
Wakiongelea kuhusu huduma za Airtel, wateja wa Airtel jiji Dar es saalam
walisema" tunafurahishwa na hufuma ya Airtel money kwani inatuhakikishia
usalama wa pesa zetu
"huduma ya Airtel Money inamgusa kila mtanzania kwani kutuma na kupokea
pesa ni kitu kisichokwepeka katika maisha yetu ya kila siku, na kama
tunavyofahamu si salama sana kutembea na kiasi kikubwa cha pesa mfukoni,
huduma ya Airtel Money ni mkombozi wa huduma za kifedha na usalama wa pesa
zetu katika maisha ya sasa. Pamoja na huduma hii kutoa usalama pia inatoza
viwango vya gharama zaidi yaani Nusu gharama inaleta unafuu na kutupatia
ziada ambayo inatuwezesha kutumia pesa hizo kufanya mambo mengine ya
muhimu" alisema Finora Fokasi mmoja wa wateja wa Airtel Money.
Kwa upande wake baadhi ya mawakala wa Airtel Money walithibitisha kuwa
'Hatoki mtu hapa' imepokelewa vizuri na wateja kwani tumeona ongezeko la
wateja katika vituo vyetu wakija kufanya miamala ya pesa . Hii nikutokana
na ukweli kwamba mteja ambaye angetozwa shilingi 7000 kutoa pesa kupitia
mitandao mingine sasa kwa kupitia huduma ya Airtel Money "Hatoki Mtu Hapa"
anatozwa shilingi 3500, niwazi kabisa kuwa punguzo la bei limekuwa kivutio
hivyo kuongeza idadi ya wateja wa Airtel Money"alisema Paulo Msangi Mkazi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...