Mshambuliaji wa Shule ya Sekondari ya BaoBab ya Bagamoyo mkoani Pwani, Zuward Ally akiwatoka mabeki wa timu ya Upendo wakati wa Tamasha la Soka la kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani 2014 lililoandaliwa na IDYDC na Grassrootsoccer kwa udhamini wa ExxonMobil, katika Uwanja wa Kituo cha Soka la Matumaini cha FIFA, mjini Iringa Mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo lilihusisha wachezaji 80 vijana wa kike wenye umri kati ya miaka 15 - 18 kutoka timu nane za Bagamoyo na Iringa. Upendo ilishinda bao 1-0. PICHA ZOTE NA JOHN BADI.
Mchezaji wa timu ya Upendo, Felista Ngimbuchi (kulia), akiwatoka wachezaji wa Shule ya Sekondari ya BaoBab ya Bagamoyo mkoani Pwani, wakati wa Tamasha la Soka la kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani 2014, lililoandaliwa na IDYDC na Grassrootsoccer kwa udhamini wa ExxonMobil katika Uwanja wa Kituo cha Soka la Matumaini cha FIFA, mjini Iringa jana. Tamasha hilo lilihusisha wachezaji 80 vijana wa kike wenye umri kati ya miaka 15 - 18 kutoka timu nane. Upendo ilishinda bao 1-0.
Beki wa timu ya Mshindo, Anifa Kalinga (kulia), akimtoka mshambuliaji wa timu ya Nianjema, Zainab Maulid wakati wa Tamasha la Soka la kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani 2014, lililoandaliwa na IDYDC na Grassrootsoccer kwa udhamini wa ExxonMobil katika Uwanja wa Kituo cha Soka la Matumaini cha FIFA, mjini Iringa jana. Tamasha hilo lilihusisha wachezaji 80 vijana wa kike wenye umri kati ya miaka 15 - 18 kutoka timu nane. Mshindo ilishinda kwa bao 2-1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...