Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo katika Ikulu ya Dar es Salaam amekabidhi vitabu 2,181 kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya vyuo vya Jeshi ili kuongeza taaluma. 
 Rais amekabidhi vitabu hivyo kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na kuahidi kuendelea kutafuta vitabu zaidi kwa ajili ya kuboresha Maktaba ya Jeshi iliyopo katika Chuo Cha Kijeshi kilichopo Monduli, Mkoani Arusha. 
 Maktaba hiyo ilianzishwa na Mheshimiwa Rais wakati alipokuwa mkufunzi katika chuo hicho miaka iliyopita. 
 "Lazima mtenge bajeti kwa ajili ya vitabu lakini na mimi nitaendelea kutafuta vitabu niwaletee ili kuijengea uwezo Library yetu ya Monduli”. 
 Akipokea vitabu hivyo kwa niaba ya Jeshi, Jenerali Davis Mwamunyange amemshukuru Rais kwa juhudi zake za kuboresha Jeshi la Wananchi Tanzania kwa ujumla na kulifanya kuwa la kisasa zaidi. 
 “Juhudi zako za kuliendeleza Jeshi letu imetuongezea uwezo na kujiamini zaidi. Bila juhudi zako tusingefika hapa tulipo na tunajivunia sana mafanikio haya” amesema Jenerali Mwamunyange .
-Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi vitabu 2069  kwa uongozi  wa Jeshi(JWTZ) kwa matumizi katika maktaba mablimbali za jeshi nchini.Wapili kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Watatu kushoto ni Mnadhimu Mkuu Jeshini Luteni Jenerali Samuel Ndomba.

-Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi na makamanda waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu 2069 kwa ajili ya matumizi katika maktaba za jeshi.Vitabu hivyo ni mchango binafsi wa Rais Katika kuboresha mafunzo ya kisasa jeshini(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tuombe mola atuletee mtanzania Kikwete kwa mara nyingine tena. Ameen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...