Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Muhidin Maalim Gurumo (mwenye shuka nyeupe) na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014, siku ambayo marehemu alizikwa kijijini kwao Masaki, Kisarawe, Mkoa wa Pwani.
Marehemu Gurumo, aliyefariki dunia juzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matatizo ya moyo, atakumbukwa kama Baba wa Muziki wa dansi nchini akianzia miaka ya 1960 na bendi mbalimbali ikiwemo NUTA Jazz na kumalizia na Msondo Ngoma kabla ya kustaafu muziki mwaka jana.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pole Bw. Abdallah Muhidin Gurumo, mtoto wa marehemu Muhidin Maalim Gurumo na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014,
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Bw. Omar Muhidin Maalim Gurumo na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014,
 Sehemu ya waombolezaji
 Mmoja wa wana familia Bw. Salim Zagar akitoa taarifa fupi ya msiba pamoja na mazishi kwa Mhe Rais
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa dansi Bwana Brighton akimshukuru Rais Kikwete kwa kwenda kutoa pole ya msiba huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. asante kwa kutoa pole

    ReplyDelete
  2. Msibawa kitaifa je rmbi rmbi zipelekwe kwa anuani ipi. Hy alikuwa kioo cha jamii ya zmn na ya ss.

    ReplyDelete
  3. Jamani Raisi wetu kwelini mtu wa watu, nampongeza kwa hilo. Muda wake wa uraisi ukiisha tutamiss katika hilo eneo.

    ReplyDelete
  4. Jk anajitahidi kwenda kuhani katika misiba ya watu mashuhuri-good for this.Lakini hembu jiulize once a month or even every 3 months, kama angezuka tu katika msiba wa MLALA HOI-asiyejulikana yeyote yule, that would be absolutely fantastic, kwani kila siku wanarudi kwenye haki watu kibao ambao hawakuwa wanajulikana kwa sababu moja au nyingine, just a thought.
    Mzee Gurumo, pumzika kwa amani and asante saana kwa muziki wato amboa ulitamba wakati nikiwa msingi na sekondari, hata kama ugali na mchicha ulikuwa haupandi, basi nyimbo zako zilifanya mchicha uwe na ladha ya nyama choma, RIP mate.

    ReplyDelete
  5. kweli kabisa BABA( JK) muda wako ukiisha tutajutaje??? wewe ni mtu wa people ,sijui atakefuata kama atakuwa kama wewe BABA we will miss you,kwa kujali tu, ni kipaji chako,i will always love you,no matter what...

    ReplyDelete
  6. Emanuel P. M.April 16, 2014

    Wadau, unapofikwa na msiba unakuwa na majonzi makubwa, ila unafarijika sana ndugu, majirani na marafiki wanapokuja kukupa pole, sasa pale
    Rais wa jamhuri ya muungano yenye wananchi milioni 45 ! na Amiri jeshi mkuu wa majeshi makini ya ulinzi na usalama ambaye pia ana mavyeo mengine kibao na tuzo mbalimbali kubwa za kimataifa anapokuja kukupa pole akavua na viatu nyumbani kwako dah......JK ingekuwa katiba inamruhusu kugombea tena mi ningempigia kura, sio kwa hili la misiba tu bali pia kwa vumbi serikali yake inalotimua katika elimu, afya, maji, umeme, barabara, utawala bora n.k.
    Mdau wa 4 hapo juu :
    1) Tafsiri ya mlala hoi ni ipi ? maana Marehemu Gurumo ( R.I.P ) alikuwa anasema yeye ni masikini japo maarufu..
    2) Nina amini kabisa kuwa JK huwa anaenda kuhani na kusalimia walala hoi wasio maarufu ila huwa hakuna media coverage ( maana kina ankal nao wanaendaga na kamera zao sehemu zenye biryani na supu ya pweza tu ) nimewahi kuona picha JK amekaa chini kwenye mkeka kwenye kajumba ka kawaida sana.
    3) Ushauri huo mzuri wa kuhudhuria misiba ya walala hoi tusiowajua uanze kwetu sisi wenyewe - je tunafanya hivyo ? maana watu hao wanatuhitaji sisi pia achilia mbali the Top Man himself..
    4) Hiyo ya mchicha kuwa na ladha ya nyama choma nakubaliana na wewe kabisaa !
    NB; Mimi sio msemaji wa Ikulu, tehetehetehe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...