Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Kashaulili, mjini Mpanda leo, baada ya kuhitimisha ziara ya siku 21ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM katika mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi.
Baadhi ya Wanachama wa CCM na wananchi wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana alipokuwa akiwahutubia wakazi wa mji wa Mpanda jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda mkoani Katavi.
Mjumbe wa NEC Taifa,Balozi Ali Karume akiwahutubia wakazi wa Mpanda mjini mapema leo mkoani Katavi,wakati wa kufunga ziara ya Siku nne ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mkoani humo.Balozi Karume aliwasisitizia wananchi hao kuwa na umoja na mshikamano katika suala zima la kuutetea Muungano,Karume akaongeza zaidi kuwa Wananchi wanahitaji Serikali mbili na si tatu kama amabvyo wengine wamekuwa wakidai.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhaman Kinana akipanda juu ya tanki alipokwenda kukagua mradi wa maji wa Ikolongo, eneo la Kazima, mjini Mpanda, Katavi leo.
Mjumbe wa NEC-CCM kutoka Zanzibar, Balozi Ali Abeid Karume (aliyevaa kofia) akipanda juu ya tanki kukagua mradi wa maji wa Ikolongo, mjini Mpanda leo

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhaman Kinana akishuka juu ya tanki alipokwenda kukagua mradi wa maji wa Ikolongo, eneo la Kazima, mjini Mpanda, Katavi leo. 

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhusiana mradi wa eneo la kuweka tanki la maji katika eneo la Kazima, mjini Mpanda, Katavi leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaidia kutandaza mabomba katika mradi wa maji wa Ikolongo, eneo la Kazima, Kata ya Kawajense, Mpanda Mjini, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM katika Mkoa mpya wa Katavi. Kinana amehitimisha leo ziara ya kikazi ya siku 21 katika mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
CCM yaendelea kuthibitisha UONGOZI BORA kwa vitendo
ReplyDeleteHongera Kinana na CCM yote.
Maina Owino
CCM UK