Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia kwa ufupi wakazi wa mji wa Karema mkoani Katavi usiku huu mara baada ya kuwasili akitokea mkoani Kigoma kwa boti na kusafiri nayo ndani ya ziwa Tanganyika takribani kwa masaa kumi na manne.Kutokana na safari hiyo kuwa ndefu ya majini,inaelezwa kuwa kuna baadhi ya Watu wamedai msafara wa Katibu Mkuu huyo umepotea ziwa Tanganyika, jambo ambalo si la kweli na la kizushi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwapungia wenyeji wake (hawapo pichani) waliofika kumpokea usiku huu kwa boti akitokea mkoani Kigoma katika bandari ya Karema mkoani Katavi,ambako amemaliza ziara yake ya siku tano na kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanal Mstaafu Issa Machibya akishuka kwenye boti usiku huu kwenye bandari ya Karema mkoani Katavi akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,na Viongozi wengine wa Taifa,Mkoa na Wilaya tayari kwa kuanza ziara ya siku nne mkoani Katavi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuka kwenye boti wakati wenyeji wake (hawapo pichani) walipokuwa wakimsubiri kumpokea usiku huu akitokea mkoani Kigoma katika bandari ya Karema mkoani Katavi,ambako amemaliza ziara yake ya siku tano na kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Viongozi mbalimbali wa mkoa na Wilaya ndani ya Mkoa wa Katavi usiku huu,alipokuwa akiwasili kwenye bandari ya Karema mkoani humo usiku huu.Kinana ameongoza na Katibu Wa NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye,Mjumbe wa NEC,Balozi Ali Karume,Mkuu wa mkoa wa Kigoma,Kanal Issa Machibya,Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Kigoma ndugu Kabouru na wengineo.
Kinana akipokelewa na Gwaride la chipukizi usiku huu ndani ya mkoa wa Katavi.
Hongera sana ndugu Kinana kwa kazi nzuri unayoifanya kuunganisha chama. Mi binafsi sijawahi kumuona katibu mkuu wa chama akitembelea hadi vijijini kama unsvyofanya. Wengi huishia makao makuu za wilaya na vijiji vilivyo karibu na miji. Kwa namna hii CCM lazima tutapata ushindi 2015. Hongera sana KM.
ReplyDelete