Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ameingilia kati Mgogoro wa ardhi uliokuwa ukifukuta kwa muda mrefu katika kijiji cha Mawenzusi,wilaya ya Sumbawanga mjini.Mgogoro huo uliohusu Wananchi na anayedaiwa kuwa Mwekezaji inaelezwa kuwa maamuzi yalikwishatolewa na Mh.Rais Jakaya Kikwete,kuwa Wananchi wapewe kipao mbele na Mwekezaji apewe kiasi,lakini mpaka sasa hakuna lililotekelezwa kufuatia Watendaji waliokuwa wamepewa dhamana ya kulisimamia jambo hilo kusua sua na hatimaye kutopatiwa ufumbuzi wa haraka.

Kinana yuko mkoani humo kwa ziara ya siku sita ya kuangalia uhai chama,miradi na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi

 Sehemu ya umati wa wananchi ukimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana (katikati) alipokuwa akiwahutubia katika Kijiji cha Mawenzusi,wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.

 Kinana alisema kitendo cha Serikali kuchukua shamba hilo na kulibinafsisha kwa Efatha bila kuwapa taarifa wanakijiji ni kuwadhulumu wanakijiji hao. "Tutakwenda kulifanyia kazi suala hili haiwezekani shamba la zaidi ya ekari 10,000 likae tu bila shughuli yoyote, Nawaambieni hivi. shamba lenu mmedhulumiwa na Serikali, hili wala haliitaji digrii 4 kujua mtu ameporwa ardhi. 

"Hapa hakuna muwekezaji kunawanyonyaji, tumeurudisha ukabaila kwa mlango wa nyuma. Ukabaila ni mtu kuchukua ardhi na kukodishia wengine", alisema Kinana. Alisema wakati Serikali inalibinafsisha shamba hilo kwa Efatha ilitakiwa wawaombe radhi wanakijiji na kuitisha mkutano wa hadhara kuwa wao wameshindwa kuliendesha shamba hilo sasa wanalirudisha kwao.

"Hao unaowaita wawekezaji wanachukua ardhi ili wakakope benki na mwisho wa siku wanawageuza wenye ardhi manamba kwa kuwakodishia mashamba", alisema. Pia,alisema Serikali imekuwa ngumu kwa kutoa uamuzi, wakati Rais Kikwete alishatoa uamuzi kuwa shamba hilo lirudi kwa wananchi jambo ambalo bado halijatekelezwa.

Alisema atahakikisha shamba hilo linarudi kwa wananchi kutokana na agizo alilolitoa Rais.Mkuu wa Mkoa aliunda tume kutokana na mgogoro huo, ambapo walibaini kuwa watu wanafanyiwa vitendo vya kikatili na kuwa shamba hilo linakaa bila shughuli yoyote na pia, ni shamba la wananchi.

"Baada ya tume hiyo kumaliza utafiti katika shamba hilo nakupitia mikataba,walipeleka maombi Serikali Kuu kuwa eneo dogo achukue muwekezaji na eneo kubwa wapewe wananchi,nitahakikisha hili linatekelezwa kwa sababu Serikali ni ngumu kutoa uamuzi", alisema.

Ndugu Kinana amemaliza ziara yake ya siku sita mkoani Rukwa kwa kutembelea wilaya zote za mkoa huo na kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi,kukagua na kuhamasisha utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi  ya chama hicho,ikiwemo na kusikiliza matatizo ya wananchi,Kinana anaelekea mkoani Kigoma ambako pia atafanya ziara.
 Mkazi wa Kijiji cha Mawenzusi, Kata ya Molo, Nuru Togwa akionesha jinsi masikio yake yalivyokatwa na anayedaiwa kuwa mwekezaji wa shamba lililokuwa la wananchi na kumilikishwa na Shirika la Chakula la Taifa (NAFCO) na baadaye shamba hilo kuuziwa mwekezaji huyo Taasisi ya EFATHA.Kulia ni Mbunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini,Mh.Aesh Hilary.
Sehemu ya Wananchi na msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakielekea kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mawenzusi,kata ya Molo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...