Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Kigoma mjini bila kujali mvua,ambapo alisisitiza kuwa CCM itatekeleza kila walichoahidi.
Kila mtu alijikinga na mvua kwenye uwanja wa Mwanga Community Centre
Viti vikitumika kujikinga na mvua iliyokuwa inanyesha wakati wa mkutano wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre wilaya ya Kigoma mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wa kwanza kulia),Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Dk. Aman Walid Kaborou, Balozi Karume na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya wakiwa wamesimama kwenye jukwaa kuu wakati wa mkutano wa hadhara bila kujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha.
Mbunge wa Kigoma mjini Mheshimiwa Peter Serukamba akiwahutubia wakazi wa Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre na kuwaambia kuwa Kigoma imebadilika na bado anapigania wananchi hao wapate maji salama na ya kutosha.
:
Mjumbe wa NEC Balozi Ali Abeid Karume akiwahutubia wakazi wa Kigoma mjini  na kuwaambia kuwa Muungano wa Serikali mbili ndio Muungano pekee utakaodumisha Umoja miongoni mwa wananchi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia umati wa wakazi wa Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre, ambapo aliwaambia kuwa vyama vya upinzani vinaelekea kutoweka mapema kabla hata havijakomaa kidemokrasia.
Upinde wa Mvua unaonekanika kabla mvua kubwa kunyesha kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre ambapo mkutano mkubwa wa CCM ulikuwa unafanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kuna ubunifu wa viti vya plastiki kugeuka miamvuli Tanzania hii ni mara ya pili ninaona hapa kwenye globu ya jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...