Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Aprili 9, 2014, kwenye Kijiji cha Kurugongo, Kata ya Kurugongo, wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Kinana yupo katika ziara ya mkoa huo kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.(Picha na Bashir Nkoromo)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasabahi wananchi wa kijiji cha Nyumbigwa ambapo alikagua mradi wa maji.
Mbunge wa Viti Maalum Josephine Gezabuke akizungumza na wananchi wakati waziara ya Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana kukagua mradi wa maji wa kijiji cha Nyumbigwa .
Diwani wa Kata ya Nyumbigwa Benjamini Chalukula akiwa amebebwa juu na wananchi wa kata yake ikiwa ishara ya kuwatumikia vizuri wakati Katibu Mkuu wa CCM alipofanya ziara kwenye kata hiyo iliyopo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Tanki la maji la kijiji cha Nyambigwa lina uwezo wa kubeba lita 290,975 na kuwahudumia zaidi ya watu elfu 11
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...