Mwalimu mkuu shule ya sekondari Mwembetogwa Kelvin Mlengule akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita kuhusiana na mabweni ya wasichana wa shule hiyo.
 Baadhi ya wahitimu wa shule ya sekondari Mwembetogwa
 Mwalimu mkuu shule ya sekondari Mwembetogwa Kelvin Mlengule akitoa taarifa ya shule kwa wazazi na wanafunzi wa shule ya sekondari Mwembetogwa katika mahafali ya 18 ya shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita akichangisha fedha kwa wazazi kwa ajili ya ununuzi wa vitanda vya mabweni ya wasichana wa shule ya sekondari Mwembetogwa. (picha zote na Denis Mlowe)

Na Denis Mlowe,Iringa

SHULE ya Sekondari ya Mwembetogwa iliyoko katika halmashauri ya Manispaa Iringa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vitanda 160 kwa wanafunzi wa kike wanaotakiwa kuishi katika mabweni yaliyokamilika katika shule hiyo.

Akizungumza katika mahafali ya 18 ya kidato cha sita na harambee ya kuchangia ununuzi wa vitanda iliyofanyika jana katika ukumbi wa shule hiyo Mkuu wa shule,Kelvin Mlengule alisema upungufu wa madawati umesababisha wanafunzi wa kike wanaotakiwa kuishi shuleni hapo kulazimika kupanga katika nyumba za watu binafsi na kuwasababisha wengi wao kujiunga katika makundi hatarishi na kupata ujauzito.

Mlengule alisema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuhakikisha wanapata vitanda kwa ajili ya mabweni ya wasichana ambayo tayari yamekwishamilika huku wakiendelea na mpango wa kujenga mabweni mengine ya wavulana wa kidato cha tano na sita shuleni hapo.

Alisema harambee iliyofanyika katika mahafali hayo wamepata mchango wa zaidi ya shilingi milioni 10 zikiwemo ahadi kutoka kwa wadau mbalimbali kati ya shilingi milioni 15 zinazohitajika kukamilisha upungufu wa vitanda na milango katika mabweni hayo.

Kwa upande wake mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Christene Ishengoma (Mb), Mkuu wa wilaya ya Kilolo,Gerald Guninita amewataka wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya kidato cha sita nchini kutumia muda uliobaki kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa kumaliza masomo yao kikamilifu.

“Vijana wangu ni vyema mkatumia muda huu mchache ulibaki kwa ajili ya kujiandaa zaidi katika kukabiliana na mtihani wenu mnaotarajia kuanza kuufanya Mei 5nkwa  kuweza kufanya vizuri na kuepuka tabia hatarishi ambazo zinaweza kuwakosesha maisha mazuri hapo mbeleni “ alisema Guninita

Guninita alisema maadili waliyofundishwa shuleni hapo ni vema wakayatumie vizuri kwa kuwa mabalozi katika jamii wanayoishi na kuepuka vishawishi na tama za kutaka vizuri kuliko uwezo wao na kuwataka kudumisha suala la nidhamu na kukataa kutumiwa na wanasiasa hususani katika suala hili linalo endelea sasa la mchakato wa kupata katiba mpya.
 
Aidha Guninita ameongeza kuwa wapo wanasiasa watako fanya mikutano na maandamano kwa kuwashirikisha vijana na kuwapatia pesa ili kuleta vurugu kitendo ambacho kinaweza kuhatarisha amani na maisha yao,hivyo wahakikishe kuwa hawajihusishi kwa namna yeyote katika vitendo hivyo.
 
Pia amewataka wazazi kushiriki kikamilifu katika kutoa michango mbalimbali ya maendeleo katika elimu,na kuacha kuchangia michango mingine isiyo na tija katika jamii zikiwemo harusi na vipaimara.
 
Katika mahafari hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa Guninita aliahidi kutoa vitanda 40 vyenye thamani ya shilingi milioni 4.8 ikiwemo ahadi yake ya shilingi laki mbili na elfu arobaini kwa ajili kununulia vitanda viwili.

Shule ya Sekondari  ya Mwembetogwa ni shule inayomilikiwa na wazazi ilianzishwa mwaka 1984 wakati huo ikiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne pekee na wahitimu waliokabidhiwa vyeti walikuwa 122 kati ya 150 walitarajiwa kuhitimu kidato cha sita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hao wasichana waliokosa pa kulala si wakuje walale kwa ghetto yangu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2014

    Michango ya sherehe nayo ina tija, vinywaji vitanunuliwa serikali itapata kodi. Ajira za muda za wapishi wapambaji wasema chochote (MC) washonaji zitapatikana. Wauza vyakula nyama, kuku, n.k watawauzia wapishi. Wenye ukumbi nao watakula. Si kweli kuwa sherehe hazina tija, watu wamejiendeleza, wakapeleka watoto shule wakajenga na kuchangia uchumi wa nchi kwa sababu tunachangiana. Zaidi ya yote ni fursa ya kukutana na kufurahia matukio ya maisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...