Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo April 28-2014, kwa ajili ya kuhutubia wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya usalama na Afya Duniani.
Afisa mkuu mwandamizi wa mazingira katika mamlaka ya Bandari Thobias Sonda akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, juu ya utumiaji wa vifaa vya kupimia hewa, wakati alipotembelea Banda la maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Mtaalam wa uchunguzi wa vyakula katika maabara ya mkemia mkuu wa Serikali Edith Wilbald akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipotembelea Banda la maabara ya uchunguzi wa vyakula kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Mtaalam wa uchimbaji wa madini katika mgodi wa Noth Mara Gold Mine Paul Kagodi akimuonesha Makamu wa Rais vifaa vinavyotumika katika kazi ya uchimbaji wa madini wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...