Oparesheni Nzito ya kuzuia Bodaboda na Bajaji zisifanye safari zake kutoka Mwenge na maeneo mengine kuelekea mjini Posta imechukua sura mpya leo baada ya Askari wa Usalama wa Barabarani kuanza kukamata Bodaboda na Bajaji zote zinazovuka Mwenge kuelekea Posta, Zoezi hilo ambalo limefanyika Mwenge Mataa Jijini Dar limeendelea kufanyika na kufamikiwa kuwanasa wengi.
Kwa mujibu wa Msemaji na Muongozaji wa Oparesheni hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kwamba wameamua kufanya hivyo ili kuzuia Msongamano wa Magari pamoja na bodaboda pia Bajaji kuelekea Mjini Posta, Aliongeza kuwa kumekuwa na uhalifu sana wa Silaha unaotumiwa na bodaboda hasa maeneo ya mjini hivyo ndio maana wameamua kuzuia.
"Tumefanya hivi ili kuepusha msongamano kuelekea Posta, lakini pia kumekuwa na uhalifu sana unaotumiwa kwa njia ya Bodaboda hivyo tunafanya oparesheni hii ili kupunguza tatizo hili. Tulicho kifanya tumewaruhusu kufanya safari pembezoni mwa mji tuu hivyo Eneo la Mwenge kwa sasa Limeingia katika zone ya eneo la Mjini,Kama tuliweza kuzuia Daladala ndogo"Hiace" pia na hawa watakuja kuelewa ingawa ni zoezi gumu na linalo hitaji elimu ya ziada ambayo tumesha anza kuwapa na tunaendelea kuwapa" alimalizia kwa kusema "Pia hii ni Oparesheni ya kawaida tuu ya kukamata wale ambao hawana Leseni za kuendesha vyombo hivi pamoja na makosa mbalimbali" alisema Polisi huyo.
Kwa mujibu wa madereva wa Bodaboda na Bajaji wamesema kwamba huo ni uonevu kuwakataza wao wasiweze kwenda Mjini kwani na wao wanatafuta ridhiki yao na wameomba Serikali iwasaidie wapatiwe njia mbadala ya wao kwenda maeneo hayo.
Wanao ruhusiwa kwenda Posta na Bajaji au Bodaboda ni wale ambao ni wamiliki binafsi na wanatakiwa wapite njia hizo wakiwa Bila abiria yoyote.
Oparesheni Kamata Bodaboda na Bajaji ikiwa inaendelea upande wa Mwenge mataa ambapo Bajaji nyingi zimekamatwa
Askari wa Usalama wa Barabarani akiwa anawaandikisha Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wenye makosa mbalimbali ili waweze kulipia tozo pamoja na kupelekwa kituo cha Polisi.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Inawezekana Bodaboda zimefanya uhalifu, lakini kwanini muwahusishe na Bajaj?. Nchi hii imebski kukimbizana na maskini barabarani na kuacha ya msaingi. Waendesha Bajaj ni vijana wasiosona, wasio na ajira, na maskini ambao wamepata ukombozi. Kwa.nini mnawakatili hata njis zao halali za kupata maisha?. Haki yao ya kuishi na kufanya kazi kujipatia kipato iko wapi?
ReplyDeleteTusije tukawasikua serikali mnsongelea swala la ukosefu wa ajira wakati mnafanya kazi usiku na mchana kuharibu ajira za watu. BAJAJ WARUHUSIWE KILA NAHSLI BORA HAWAVUNJI SHERIA
Serikali isimamie hapo hapo mambo ya bajaji na bodabodo ziishie huko huko kwani ajali nyingi kwa sasa zinatokana na hivi vyombo vya usafiri wanaendesha bila kufuata sharia, mie nashuhudia wakati zikiingia mjini kwa siku lazima nione ajali zaidi ya moja na ni hawa hawa bodaboda. Mji unakuwa hauna mpangilio wa matumizi ya barabara ni kwa waendesha magari na hao bodaboda. Ziishie huko huko kupunguza ajali za ovyo huku mjini!
ReplyDelete