Jenerali Mella, Kamanda wa Jeshi la UNAMID akibadilisha mawazo na Balozi Mwinyi, ambapo pamoja na mambo mengine, amesema wanajeshi kutoka JWTZ ambao ni sehemu ya UNAMID wameendelea kuonesha weledi na kujituma kwa hali ya juu katika eneo la ulinzi wa amani, ulinzi wa raia na usimamiaji wa misaada ya kibinadamu. Akasema kutokana na mapingano ya kikabili yanajitokeza mara kwa mara, na kuwa sehemu kubwa ya mapigano hayo yamekuwa yakitokea katika maeneo zilipo kambi za wanajeshi kutoka Tanzania, wanajeshi wetu wamejikuta wakilazimika kutoa huduma mbalimbali zikiwamo za kuwazalisha wanawake waja wazito. Utoaji wa huduma hiyo ya uzazi salama nje ya mamlaka yao imewafanya wazazi waliojifungua kuwapatia majina ya kitanzania watoto wao, kama shukrani yao kwa madaktari hao wa kitanzania kwa kuokoa maisha yao na ya watoto wao. Kushoto kwa Jenerali Mella, ni Luteni Kanali, Wilbert Ibuge, Mwambata Jeshi katika Uwakilishi wa Kudumu
Luteni Jenerali Paul Mella, Kamanda wa Jeshi la Mseto la Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika Darfur ( UNAMID) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ( hayupo pichani). Jenerali Mella alifika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kufuatia ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika Umoja wa Mataifa ambapo alikuwa na mazungumzo na Wakuu mbalimbali wa UN. Akielezea tathmini yake ya miezi nane kama Kamanda wa UNAMID Jenerali Mella anasema njia pekee ya kupatikana kwa amani ya kudumu katika jimbo la Darfur ni kwa pande zinazopingana kukaa katika meza ya mazungumzo na kumaliza tofauti zao.

Na Mwandishi Maalum

Kamanda wa Jeshi la Mseto la Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika Darfur ( UNAMID) Luteni Jenerali Paul Mella, amesema, mazungumzo yatakayozihusisha pande zote zinazopingana katika mgogoro na machafuko yanayoendelea katika Jimbo la Darfur ndiyo suluhu pekee inayoweza kurejesha hali ya Amani, usalama na utulivu katika jimbo hilo.

Jenerali Mella, ameyasema hayo wakati alipokuwa akibadilishana mawazo na Balozi Ramadhani Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wakati Jenerali Mella alipoutembelea Uwakilishi wa Kudumu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...