Wakati bunge Maalum la Katiba linaendelea na kikao leo, baadhi ya wajumbe waliokuwa wanasemekana kuwa ni wanachama wa umoja wa kinachoitwa katiba ya wananchi (UKAWA) wamejitokeza na baadhi yao kukanusha kuunga mkono umoja huo.
Mmoja wao ni Mhe Ezekiel Oluoch ambaye alikuwa anadaiwa kuwa miongoni mwa WANA UKAWA aliingia Bungeni jana na kukana kuhusika na umoja huo na kuongeza kuwa yeye hana kundi lolote ndani ya bunge, na kwamba ataendelea na kazi ya aliyoteuliwa kuifanya.
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Mhe. Ezekiel Oluoch akiingia jana kwenye kikao cha Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Mhe. Uluoch, ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa Chama cha Walimu (CWT), ni mmoja wa wachangia mada wakubwa aliyejipatia umaarufu mkubwa mjengoni.
![]() |
Mhe. Uluoch akisimama kutoa ufafanuzi kuwa yeye hana kundi bungeni humo. |
.jpg)
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la KAtiba Mhe.Samwel sitta akiliambia Bunge jana kuwa pamoja na UKAWA kuondoka koramu ya wabunge walio ndani ya ukumbi imetimia kwa hiyo mchakato wa katiba mpya utaendelea kama kawaida.
Hii inafuatia kikundi kinachojiita umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) kususia Bunge wiki iliyopita, na baada ya baadhi yao kurudi na kuendelea na bunge kama kawaida.
Wanaoendelea na bunge wengi ni kutoka kundi la wateule 201 na baadhi ya vyama vya upinzani ambao mwanzo walionekana kuunga mkono UKAWA.
Na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa
Photo Solutions Wawakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati.
Rejeeni mshiriki katika mchakato wa kutengeza katiba ndugu zetu. Bado tunalia na hekima wakati wa kuchangia hoja. Bado hekima inatakiwa katika kutoa hoja.Tuheshimu hivi vikao tafadhali.
ReplyDeleteThe mdudu,ndugu zangu tumieni busara kidogo jamani hao waliosusia sio watt wadogo ni watu na akili zao timamu,why nasema hivi? Ndugu zangu kadili mnavyoendelea na vikao bila ya hao UKAWA wananchi wataona kama hiyo katiba imeegamia upande mmoja jamani waiteni hao kiustaarabu watarudi hao,mm naona mbali sn mwezenu na nimejawa na busara tele kabisa moyoni tutengenezeni KATIBA isio na manung'uniko.
ReplyDelete