Mike Lukindo enzi ya uhai wake.
Watanzania wa Wisconsin wanapenda kutoa shukurani kwa wote waliojaribu kuokoa kutokuchomwa moto kwa ndugu yetu, mpendwa wetu Mike Lukindo na pamoja na jitihada zote zilizofanyika tunasikitika kuwataarifu kwamba mpendwa wetu ilibidi achomwe moto na jana Ijumaa April 4, 2014 majivu yake walikabidhiwa familia yake kwa mtoto wa kwanza wa marehemu kwenda kuchukua majivu hayo. Mpaka mazishi yafanyike zilikua zinahitajika $6,000 pamoja na michango ya sisi tuliopo Madison, Wisconsin haikuweza kufikia idadi iliyokua inahitajika.
Watanzania wa Wisconsin wanawashukuru vyombo vya habari ndani na nje ya Marekani vilivyosaidia kusambaza habari ya ndugu yetu, mpendwa mwenzetu na Mtanzania mwenzte mpaka habari kuwafikia ndugu zake Tanzania.
Shukurani za pekee kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani hususani Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwa mchango waliotoa na mara kwa mara Balozi kupiga simu kufuatilia maendelea ya msiba.
Sisi Watanzania wa Wisconsin kwa niaba ya familia tunasema asante na mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atawazidishia, Asanteni.
daah,R.i.P.
ReplyDeletetuliambiwa ahera kuna moto sasa kuchomwa hapa duniani huyu bwana kaadhibiwa kabla ya hukumu
Sasa uraia pacha wa nini iwapo hio pesa kiduchu tu mmeshindwa kuichanga..hivi nyie kweli ni watu wa kuwekeza bongo?? au ndo mnachotaka ni kwenda bongo kudandia vyeo vya CCM tu???hiko chama cha watanzania na matawi kibao ya ccm na chadema yanawasaidia???kama mnashindwa kuraise only 6000US dollars?? RIP Mike.
ReplyDeleteMdau wa Finland.
What does this have to do with dual citizenship? Do you even know what dual citizenship is? Fyi i dont support it. If you dont research you have no right to speak
DeleteUliyetuma huu ujumbe wewe mzabizabina, ndiyo maana hata hukuweka jina lako ni nani, kuna post ya awali iliwekwa hapa kwamba marehemu mwenyewe aliaumua ya kwamba atachomwa kama atatangulia kenye haki.
ReplyDeleteMarehemu alikuwa na mke na watoto, hopefully alikuwa ameandika WILL, na kama ni kuzika au cremation ni maamuzi ya mkewe na watoto wako and nobody else!
Ulivyoandika kama vile kuchoma ni jambo baya na la kimasikini, wakati huku uhaibuni ni kitu cha kawaida kutokana na matakwa ya marehemu mwenyewe na wanafamilia, mama yake Obama alikuwa cremated, babu na bibi yake pia kadhalika, sasa usiwapotoshe watu hapa kwamba huyu marehemu amekuwa cremated kwa ukosefu wa hela, kwani cremation also cost money.
Tujitahidi tusiingilie mambo ya kifamilia eti kwa sababu huku bongo wanaochoma ni baniani peke yao.
Marehemu apumzike kwa Amani-Amen.
Watanzania bwana kwa kuingiza siasa kwenye kila kitu hatujambo. Huu msiba ulikuwa tayari kila kitu kimepangwa na marehemu pamoja na familia yake walitaka marehemu azikwe kwa njia ya cremation, nyie ndio mnaita kuchoma moto.
ReplyDeleteMke wa marehemu alitaka kuwajulisha tu ndugu zake marehemu wa Tanzania kuwa ndugu yao amefariki na wanamzika, sasa nyie mkandandia train kwa mbele.
Ndio, sasa kikatokea hichi kikundi au jamaa wanajiita 'watanzania wa madison' na kuanza kuingiza siasa eti wanachangisha $6000 'kumnusuru' marehemu eti 'asichomwe' jamani hamna hata soni kutaka amri ya marehemu ya kuwa cremated isitimizwe wakati nyie hata sio familia?
Halafu Marehemu ni mmarekani mwenye asili ya tanzania sasa nyie mlitaka kuingilia mambo ya familia kwanini?
Mungu ni mkubwa sasa nyie ndio mmepata aibu kutaka kuingilia mambo ya kifamilia, liwe fundisho kwa wengine.
Nadhani kuna haja na kuitazama vizuri hoja ya wanadiaspora ya kuja kuwekeza bongo iwapo watapatiwa uraia pacha....
ReplyDeleteTHE WAY I SEE here is people like to waste their time with physical things which are temporary. The physical body is temporary. The real man is the spirit which had already departed the day he died. the body is jusy the shell. Accept christ nowso u can live forever.
ReplyDeleteAmen.
Jamani narudia tena wakati wa vilio vya watu si wakati wa kuleta siasa zetu mdau #2 na mdau#5, hekima itwale.
ReplyDeletePia kama mnategemea Diaspora waje wawatatulie matatizo yenu ya kuwekeza,mtangoja sana. Mnadhani wabongo kwa vile wako diaspora watawafanyia kazi nyie, halafu mnaongea pumba juu yake, poleni sana.
Tatu, kama nyie mna hela za kuchangia kila kitu changieni basi, mnajua kuchonga sana mdomo, vitendo sifuri. Diaspora ni haki yao kuwa raia wa Bongo kwa vile wamezaliwa hapo, mwisho wa habari.
diaspora hawa hawajielewi wala hawazielewi haki za muafrika akifa sio kuchomwa moto. uyahudi,ukiristo na uislamu dini hizo zote zinakataa na sisi waafrika ndio wafuasi wa dini hizo wengi wetu, lakini unapokwenda uhaibuni na ukajikubalisha kama wewe unataka uwe miongoni mwao yaani uwe raia wa huko hio inatosha kwa wewe kuwa wa huko na huku TZ musahau tena. hivyo kuzikwa kwa namna hio ni sahihi kwa marehemu maana amechagua style ya maisha hao kipindi chan uhai wake, MKO SAWA. LAKINI CHENGINE NAIOMBA TANZANIA ISIKUBALI WAZO LA URAIA PACHA HII NI HATARI KWA USALAMA WA TAIFA LETU LENYE RASILMALI ZINAZOSIMAMIWA WA WATU WASIO NA ELIMU NA UZOEFU WA KUTOSHA. DIASPORA NDIO WANAOLETA KILA AINA YA FITNA NCHINI HATA ZA UMWAGAJI WA DAMU SABABU BAADHI YAO WANATUMIWA KUWA VIBARAKA KWA TAMAA YAO YA KUPATA MAISHA MAZURI NA YASTAREHE. UKIAMUA MOJA IWE MOJA TENA MBILI YANINI????????????
ReplyDeleteDIASPORA HAWANA HAKI KIKATIBA YA KUWA RAIA WA TANZANIA.
ReplyDeleteKWANZA HAWA DIASPORA NI OMBA OMBA WALIKIMBIA BONGO HALI ILIPOKUA MBAYA SISI WAZALENDO TUKASTAHAMILI HALI NGUMU YA MAISHA. SAIVI WANAONA BONGO INAKUWA WANAJITIA KUDAI DUAL CITIZENSHIP WASIKUBALIWE HAWA KWENYE MCHAKATO WA KATIBA MPYA. TUNAWAPENDA WAJE TANZANIA KAMA NI WAGENI-WENYEJI ALAFU WARUDI KWAO.
Msibishane nyie msiopenda kusoma hapo juu. Hebu rudini ktk historia ya baba yetu Adam watoto wake KABIL na HABIL walipo pigana mmoja akamuua mwenzake hakujua la kufanya, bali alifundishwa na kunguru wawili nao walikuja mbele yake wakapigana na mmoja akamuua mwengine, badae yule kunguru alieshinda akachimba kashimo kwa miguu yake na kumzika mwenziwe. hapo ndipo binadamu tulipojifunza jinsi ya kumsitiri kiumbe pindi anapofariki, hii ndio haki ya utu. je marekani hakuna ardhi ya kutosha kwa ajili ya mtu au binadamu kuzikwa. me naona sio kweli bili sisi viumbe tunapenda haki ya uhai zaidi kuliko kufa. tabia nyengine ambayo vimbe tunayo ni kupenda kubadilisha sheria za Kimaumbile maana kila kiumbe kimepewa haki na wajibu wake hapa duniani, "mfano ardhi moja kati ya haki na wajibu wake ni kuwameza viumbe au watu wote pindi watakapokufa other things remains constant" moto pia una haki na wajibu wake lakini haukuamrishwa kuwachoma wafu unless other wise. lakini mfano halisi ni kuhalalisha ndoa za jinsia moja???????????? jee hii ni haki na wajibu wa viumbe kuingiliana kwa namna hio???????. sasa mm naona diaspora wasipewe uraia wabakie huko huko. nnayo mengi lakini hayo ni machache kama ni ukumbusho
ReplyDeletekuchoma "cremation" ni uamuzi wz familia na alivyotaka marehemu Ughaibuni Cremation ni jambo la kawaida, si suala la uwezo. Mwenzetu ametutoka tuanduke mema wakati huu wa huzuni. R.I.P Mike
ReplyDeleteKinachosikitisha ni kwamba yalitolewa matangazo mengi ya kuomba mchango wa $ 6,000 ili huyu bwana azikwe badala ya kuchomwa. Waliotoa matangazo walisema wasingependa achomwe moto! Kwa hiyo kuchomwa kwake ni matokeo ya kukosa hizo $ 6,000 na si wosia wake. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen.
ReplyDeleteMSICHOELEWA NINI NYIE WABONGO MSIOTAKA KUELEWA? KUCHOMA MWILI HUKU MAREKANI SIO AJABU NI JINSI MTU ANAVYOTAKA SASA NYIE MNATAKA MNAVOTAKA NYIE NANI? NA HUO URAIA MNAOJIFANYA ETI TUSIWE NAO NDIO UTAWAPELEKA WAPI?WATU WENGINE BWANA!YAANI WATANZANIA TUNAJULIKANA KWA UCHOYO NA UBINAFSI, WALA HAMNA CHA AJABU YAANI MNAFIKIRI WATU WAKIPATA URAIA PACHA NYIE MTAKOSA NINI KAMA SIO KUKOSA BUSARA TU. UCHOYO TU NA UBINAFSI TUNAWAJUA.SIZITAKI MBICHI HIZI.
ReplyDeleteMdau wa nne juu yangu ameongea vzuri kuwa kuchomana moto sio asiri yetu binadamu coz hakuna dini hata moja inayosapport swala hilo....bad enough nashangaa nyie wana diaspora mnavyozid kusaport hiyo western culture ya cremation..!
ReplyDeleteHivi mkiruhusiwa hiyo dual citizenship c mtatuletea huo utamaduni wa kuchomana huku nyumbani...?
We love u so much ndugu zetu but katika hili napinga hiyo dual citzenship..na mbaki tu kuwa wagen huku tz.
Hahahaha!wabongo utawajua tu kwa uchoyo, roho ya korosho na wivu, kwani situnakujaga bongo, yaani bado maukiritimba kibao mijitu kujifanya miungu mtu na roho mbaya ndo maana mnapinga diaspora wasipewe dual, Ok sisi ni watanzania na tutabakia hivyo na hizo passport za kijani tunazo so please shut up guys kaeni na roho zenu mbaya kisa mnaishi kwenye shida Mara mavumbi mara mafuriko mara magonjwa kibao mara mammbu kila kona mra mainzi kila kona, but still home no home tuna ndugu zetu huko and we wanna contribute to me things better for u guys
ReplyDeleteYaani humu kwenye mitandao kweli tunaongea na misukule. Mdau anasema "DIASPORA NI OMBA OMBA WALIKIMBIA BONGO HALI ILIPOKUA MBAYA SISI WAZALENDO TUKASTAHAMILI HALI NGUMU YA MAISHA. SAIVI WANAONA BONGO INAKUWA WANAJITIA KUDAI DUAL" kwa hiyo sisi wote lazima tubanane Bongo?!! Basi kama ni hivyo na walio mikoani wasingekuja Dar es salaam(Maana Dar ni mchangayiko). Yaani jamaa pointless kabisa. Naona jamaa wanaandika humu ili mladi basi tu au wawakasilishe watu. Ndugu Michuzi mie na sapoti kutuachia kama zamani tuchafue hali ya hewa. Maana kuna mida inabidi mtu utukane tu kwa sababu watu wanarudia kuongea pumba.
ReplyDelete