Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, akizungumza na ujumbe kutoka African Medical Research Foundation (AMREF) ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi hiyo hapa nchini Dr. Festus Ilako. Mama Salma alikutana na ujumbe huo ofisi za WAMA tarehe 11.4.2014.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya kushawishi wake wa Marais wa Afrika katika kutetea haki za wanawake na watoto ili kupunguza vifo vya akina mama na watoto “ Stand Up for African Mothers”. Anayekabidhi tuzo hiyo ni Mkurugenzi Mkazi wa AMREF hapa nchini Dr. Festus Ilako. Sherehe hiyo ilifanyika kwenye ofisi za WAMA tarehe 11.4.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kkwete akiongea na ujumbe kutoka AMREF mara baada ya kumkabidhiwa tuzo ya “Stand up for African Mothers” tarehe 11.4.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera saana 1.Lady Mama Kikwete umefanya kazi kubwa saana katika
    maendeleo ya kina mama Tanzania
    na bara zima la Afrika.
    Haswa zaidi utakumbukwa kwa moyo wako wa imani kuzisimamia taasisi zote za malezi ya watoto yatima.

    Mikidadi-Denmark

    ReplyDelete
  2. Mama hongera sana. Hamasisha ujenzi wa kisasa wa michezo kwa ajili ya wasichana. Watakukumbuka. Ukiamua unaweza. Si unaona hiyo pete?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...