Chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) kimefanya mkutano mkuu wa kawaida kwenye ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Kagera na Mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Missenye Kanal Issa Njiku.
Awali akisoma taarifa yake mwenyekiti wa KRFA ambae pia ni Rais wa TFF Jamal Emil Malinzi aliwashukuru wajumbe wote wa mkutano mkuu kwa namna walivyoshiriki kwa namna tofauti katika kuendeleza michezo katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera,Hotuba iliyosheheni mipango kedekede ya kuinua soka kwa ujumla nchini Tanzania na Kagera ikiwemo.
Katika mambo mengi aliyoeleza ameweza kueleza changamoto nyingi zinazoikabiri KRFA na kuwataka viongozi kuhakikisha wanawasiliana na Halimashauri za wilaya zao kutenga maeneo ya viwanja vya michezo,akiongelea uwanja wa Kaitaba amesema anayofuraha kuwajulisha wajumbe kuwa sasa uwanja huo unawekewa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA kwa asilimia mia moja, Lakini pia amehaidi kuitisha Harambee ya wadau mbalimbali jijini Dar es salam kwa ajili ya kupata pesa ya kujenga jukwaa moja katika uwanja wa Kaitaba Bukoba.
Pia aliweza kuelezea kuhusiana na nafasi ya Uenyekiti wa KRFA, Amesema tangu amepata nafasi ya Rais TFF amekuwa akikutana na maswali mengi ya waandishi wa habari na wadau kuhusiana na kujiudhuru nafasi hiyo, (Wakati nakuja Bukoba nilikuwa na wazo ili la kujiudhuru, Lakini kila mjumbe aliesimama hapa ameniomba nisijiudhuru mpaka wengine kutamka kuwa iwapo nitajiuzuru basi nao watajiudhuru nafasi hii, lakini kuna mjumbe kasema wapo watu wakati wa kampeni walikuwa wakisema natafuta nafasi hii ili niweze kugombea urais, kwahiyo basi naomba nitamke kuwa sitojiudhuru nitaendelea kuwa mwenyekiti wa KRFA.)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...