Mpiga
Gitaa wa Skylight Band maarufu kwa jina la Chiri Challa(pichani)
amefariki dunia usiku wa kuamkia April 17 katika Hospitali ya Muhimbili.
Taarifa
za awali zimethibitishwa na uogonzi wa bendi hiyo kuwa mpiga gitaa huyo
machachari amefariki baada ya kuugua kwa siku mbili ugonjwa wa kupooza
nusu ya mwili wake na kuepelekea kutofanya kazi ipasavyo.
Kwa
mujibu wa Meneja wa bendi hiyo Aneth Kushaba AK47 Ugonjwa wa kupooza
ulipelekea mishipa ya damu kichwani kupasuka hivyo na kumsababishia
maumivu makali sehemu kichwani.
Kutokana
na msiba huo uongozi unapenda kutoa taarifa kuwa Show ya Escape One
iliyokuwa ifanyike Alhamis ya April 17 imeahirishwa hata hivyo uongozi
unasikitika kumpoteza msanii huyo ambaye alikuwa ni kiungo muhimu wa
bendi na inaungana na familia ya marehemu Chiri Challa kuomboleza kifo
cha mpendwa wao na inatoa pole kwa familia na mashabiki wa Skylight Band
na wapo bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.
Msiba na shughuli za mazishi zinafanyika maeneo ya Mwanyamala Ujiji mtaa wa Mpunga.
Kwa mawasiliano zaidi namba ya Meneja wa Bendi
+255 715 677 499.

RIP mate, most likely cause of death is subarachnoid haemorrhage, the main cause being aneurysm rupture.
ReplyDelete80% of cases are due to "congenital" / berry aneursym - peak age from 40 to 50 years of age.
Mgonjwa atapata maumivu makali sana ya kichwa amabayo yanaanza ghafla.
sudden severe headache ("my worst headache ever").
Hemiplegia will happen depending on the site of the bleed.
Nikiwa high school one chap Manyerere RIP died suddenly with severe headache, alisema kichwa kinauma sana kama mtu amempiga kichwani vile, akaanguka na kuaga dunia, watu wakasema katumiwa jinni huyu, I got the answer in medical school SAH.
RIP,