Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti), akikata utepe kuzindua rasmi mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, Kata ya Msongola, Wilayani Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). Wa pili kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo, Diwani wa Kata hiyo, Bi. Angelina Malembeka na Ofisa Mauzo wa TBL Ilala, Bw. Godrack Kalebi.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti kulia), akiondoa kitambaa kuzindua mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), anayemsaidia ni Ofisa Mauzo wa TBL Ilala, Bw. Godrack Kalebi. Wanaoshudia ni Mkuu wa Mahusiano wa TBL, Bw. Stephen Kilindo na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Dkt. Asenga Severin.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti), akijaribu kufungua koki ya bomba la maji, baada ya kuzindua mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, iliyoko Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, kilichojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). Wa pili kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo, Ofisa Mauzo wa TBL,  Ilala, Bw. Godrack Kalebi na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Bi. Doris Malulu.
 (mwenye suti), akisaidia kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Mvuti, Bi. Aghata Senga, baada ya kuzindua mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, iliyoko Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, uliojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). kulia ni Mkuu wa Mahusiano na sheria wa TBL, Bw. Stephen Kilindo, Ofisa Mauzo wa TBL kanda ya Ilala, Bw. Godrack Kalebi (wa pili kulia) na Diwani wa Kata hiyo, Bi. Angelina Malembeka (mwenye kilemba kushoto).
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti), akimshika mkono wa pongezi Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Doris Malulu (wa pili kulia), wakati wakielekea kuzindua mradi wa maji katika zahanati ya Mvuti, iliyoko Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam jana, ulichojengwa na TBL. Kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...