Na Greyson Mwase, Ujerumani

Waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano litakalofanyika kesho Berlin nchini Ujerumani ambapo atawasilisha mada kuhusiana na fursa za uwekezaji nchini Tanzania hususan katika sekta ya mafuta na gesi.

Kongamano hilo litakaloshirikisha wasomi mbalimbali litaenda sambamba na maonesho yatakayooneshwa na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini kama moja ya maadhimisho ya jubilee ya miaka 50 ya muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha Prof. Muhongo Ujerumani, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo alisema kuwa mbali na mada itakayowasilishwa na Prof Muhongo mada nyingine zitakazowasilishwa ni pamoja na fursa zilizopo katika sekta ya madini, kilimo, viwanda ikiwa ni pamoja na utalii, uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Ujerumani na nafasi ya lugha ya Kiswahili katika kuimarisha umoja.

Balozi Marmo aliongeza kuwa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano baina ya Tanyanyika na Zanzibar yatahudhuriwa na wawakilishi kutoka balozi mbalimbali na watanzania waishio nchini Ujerumani.

Balozi Marmo aliongeza kuwa katika historia ya nchi ya Tanzania ukoloni uliacha mambo ya kukumbukwa kama vile miundombinu ikiwa ni pamoja na mashule na mahospitali.

“Pamoja na changamoto katika ukoloni lakini umeacha alama za kukumbukwa hususan katika suala zima la miundombinu. “ Alisisitiza Balozi Marmo.
Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo (kushoto) akisisitiza jambo wakati akimkaribisha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ( aliyekaa upande wa kulia).
Afisa Mkuu wa Utawala na Fedha katika ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani Bw. Caesar Waitara akifafanua jambo katika kikao hicho.
Baadhi ya washiriki watakaoshiriki maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanyanyika na Zanzibar wakimsikiliza kwa makini balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo (hayupo pichani).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...