Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kundi la Wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa walio marafiki wa Tanzania pamoja na wanachama wa Britain and Tanzania Society (All Party Parliamentary Group on Tanzania, and Britain Tanzania Society) katika mchapalo walioandaa kwa heshima yake katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola katika jengo la Durbur jijini London April 1, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na baadhi ya Wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa vya Uingereza walio marafiki wa Tanzania pamoja na wanachama wa Britain and Tanzania Society (All Party Parliamentary Group on Tanzania, and Britain Tanzania Society) katika mchapalo walioandaa kwa heshima yake katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola katika jengo la Durbur jijini London April 1, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akijaribu kuendesha mfano wa mtambo wa kufundishia namna ya kuchimba mafuta katika visima vilivyo bahari kuu (KCA Deutag Dart Drilling Simulator and Well Enginering System) alipotembelea Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland, Jumanne April 1, 2014 akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kiserikali ya siku tatu nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron. Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho kuanzia mwaka huu, ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi. Nyuma yake ni ujumbe alioongozana nao ikiwa ni pamoja na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui (kulia) na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo (wa pili kulia) Wa pili kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe Peter Kallaghe, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya katika Wizara za mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Balozi Dorah Msechu.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland, Jumanne April 1, 2014 akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kiserikali nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron. Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho mwaka huu, ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo wakisindikizwa na Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland, Jumanne April 1, 2014 alikotembelea akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kiserikali nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron. Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho mwaka huu, ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi.PICHA NA IKULU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. tunaomba serikali ya uingereza ihakikishe hizo nafasi za kusoma zinagawiwa sawa kwa sawa baina ya tanganyika na zanzibar , vinginevyo zote zitachukuliwa na tanganyika , na sisi znz mafuta tunayo kama watanganyika watatupa uhuru wetu tutajitanua na sisi kwa mafuta , yahooooooooooo

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza mi nadhani kilicho bora kwako ni kuomba s.tatu ili ujinafasi pia kupunguza lawama.

    ReplyDelete
  3. wewe uliyeandika hapo juu angalia sana ,wewe utasemaje nafasi zigawiwe sawa,huko hakuna kufuata usawa wanaenda wenye sifa na kama hakuna wenye sifa wakifuata usawa si itakuwa kama bunge la katiba wamefuata usawa huko wanapigiana kelele kama wazanzibar watachukuliwa kama watanzania wengine tu na kama hakutakuwa na na wenye sifa za kwenda hata mmoja haendi au na sie wasumbawanga tuseme lazima wafipa waende kusomea mafuta,wazanzibar wataenda zikija nafasi za uvuvi.

    ReplyDelete
  4. Huu muungano wa kulazimisha utatuletea shida sana. Na bado mafuta hayajapatikana!

    Mgaibuni

    ReplyDelete
  5. Mdau wa 3 umetoa ufafanuzi mzuri sana:

    Hatuwezi kufika kama tuta endekeza dhana ya ubaguzi kati ya Bara na Visiwani.

    KIGEZO CHA NAFASI ZA KUSOMA MASUALA YA MAFUTA NA GESI NI,

    ''RAIA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MWENYE SIFA ZINAZO HITAJIKA KIMASOMO''...FULL STOP!

    ReplyDelete
  6. Wandugu zetu wa Visiwani wa-Zanzibari inaeleweka mnaifahamu Dini vizufri sana.

    Nadhani mnaelewa ya kuwa watu wamegawanyika kati ya Makundi mawili makubwa, Kuna NAFSI LAWWAMA na NAFSI MUTUMMAINA,

    Sasa weni wenu nini ni NAFSI LAWWAMMA mtalalamika njaa mkipewa shibe mtakula hadi mnavimbiwa mtaendele na lawama mmevimbiwa!

    Lipi jema kwenu ninyi NAFSI LAWWAMMA?

    ReplyDelete
  7. Mdau hapo juu yani wewe kwa akili zako unaona kuwa Visiwani hakuna anayefaa au ni upendeleo tu.

    ReplyDelete
  8. mdau wa kwanza bila ya zanzibar kupewa uhuru wetu sahau mambo ya usawa.mdau wa pili huo usawa ndo utaletwa na hizo serikali 3 kwa kuing'ang'anua tanganyika ktk koti la muungano.nafasi za tanganyika mtajuana wenyewe kama waende wafipa,wachaga,wasukuma nk,kule znz nako watajuana kama waende wamakunduchi,wakengeja,watumbatu,wamtambwe nk.zanzibar na tanganyika kwanza.tumechoka kutawaliwa.

    ReplyDelete
  9. Acheni UBAGUZI na UPUMBAVU nini Wanzazibari!

    Kila kitu ohhh Wazanzibari!

    Kila azimio likiwekwa mezani ohhh Wazanzibari!

    Hivi Marehemu Abeid Aman Karume na Marehemu Julius Kambarage Nyerere wangukuwa na vichwa vya 'panzi' kwa upeo mdogo na finyu wakufikiri kama ninyi mnafikiri sijui tunge kuwa wapi?

    ReplyDelete
  10. Wazanzibari msitegemee kubebwa kila sehemu!

    Nafasi zitatolewa kwa kuzingatia Sifa za Ufaulu wa Masomo na uwezo wa Kiakili!

    Msifikiri kwa sababu Masomo yatatolewa huko Uingereza mtaitumia nafasi hiyo kwenda UK na mkajilipue Ukimbizi hiyo haita wezekana mkae mkijua!

    ReplyDelete
  11. Sio Wazenji mfosi kupewa nafasi za Masomo UK halafu mkifika mkabebe Maboksi badala ya kusomea Masomo ya Gesi na Mafuta!!!

    ReplyDelete
  12. Wazanzibari mpo kwenye ''JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA''

    Kama mnavyo fahamu ya kuwa nchi yetu ni kubwa sana (SIO KAMA RWANDA UNAYOWEZA KUIZUNGUKA KWASIKU MOJATU), kutokea huko Visiwani hadi Mbeya, Shinyanga na Kibondo ambako ndugu zetu wa kutokea Kisiwani Pemba wana jishughulisha na shughuli zao za kilimo cha mpunga na ukataji wa Mbao (KULINGANA NA WAO WAPEMBA KUTIMIZA MASHARITI YA KUFANYA SHUGHULI HIZO ZA KILIMO NA MBAO NCHINI), VIVYO HIVYO NAFASI ZA MASOMO YA GESINA MAFUTA ZITATOLEWA KWA KUZINGATIA UKUBWA WA NCHI NA MGAWANYO WA WATU,SIFA ZA ELIMU NA UWEZO NA SIO KIUBAGUZI KI-BARA NA KI-VISIWANI!!!.

    ReplyDelete
  13. INATISHA SANA LAKINI IMESIKIKA MSOMI MMOJA AKISEMA
    "VIONGOZI NA WANASIASA WANAPOSEMA TUULINDE NA KUUDUMISHA MUUNGANO WANAMAANISHA MUUNGANO UPI?WALIOTUACHIA WAASISI WAKE YAANI NCHI MOJA SERIKALI MBILI AU ULIOPO SASA WA NCHI MBILI SERIKALI MBILI BAADA YA ZANZIBAR KUFANYA MABADIRIKO YA 10 YA KATIBA YAO?"
    NDO HALI HALISI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...