Ndugu zanguni,
Tunapenda kuwapa habari njema watu wote kuwa kuanzia tarehe 01/05/2014 Kampuni yetu inayomilikiwa na Watanzania waishio UK, inahamishia ofisi zake ndani ya bandari kubwa kuliko zote za kusafirisha magari UK , PORT OF TILBURY.
Sisi tutakuwa weusi wa kwanza kabisa kupewa ofisi ndani ya hii bandari na hivyo majina yetu kuingia kwenye historia. Na serikali imetukubali baada ya kuona jinsi tulivyoweza kujibeba kutoka kwenye kiosk mpaka tulipo.
Mkumbuke Serengeti ilianzishwa kwa mtaji wa £1,800 tu.
Tumepewa mkataba wa miaka 10 na tunaweza ku-renew baada ya hapo kama bado tutakuwa tunataka kuendelea na biashara ndani ya bandari
Tumechukua Yard yenye ukubwa wa ekari mbili na ofisi yenye ukubwa wa 2,500sq ft.
Hii itatusaidia kuboresha huduma zetu kwa sababu tuna mpango wa kukodi meli ya saizi ya kati ili magari yetu yote na makontena tuwe tunasafirisha wenyewe na pia kusafirisha magari na makontena ya makampuni mengine pia.
Pia usalama wa mali za wateja ni maximum kwa sababu kuna zaidi ya camera 5,000, kituo cha polisi ni hatua mia tatu tu kutoka kwetu, police patrol ni 27/7
Yard /ofisi zetu zitakuwa OPPOSITE BERTH 31, BESIDE HYUNDAI TERMINAL
Tukiishakamilisha mkataba wa kukodi meli tutatoa punguzo kubwa kwa usafirishaji wa magari kwa asilimia 40% ili kurahisisha watu kuweza kuagiza magari yao toka UK kwa bei nafuu. Pia tutakuwa tunatoa free storage kwa magari na free loading.
Kama kuna mtu ana kitu au mzigo ndani ya ofisi zetu za sasa tunaomba aje achukue sababu hatutahama na mzigo wa mtu
Wote mnakaribishwa.
CHRIS LUKOSI
Managing Director
SERENGETI FREIGHT
WE ARE OPEN ON SATURDAY 10:00-18:00HRS
WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
Tupigie kwa namba hizo hapo chini au tutumie email tafadhali
CHRIS LUKOSI +44 (0) 790 38 28 119 OR +44 (0) 7404 27 96 33SIMON LOUIS +44 (0) 79 506 89 243
Tell (+44) 01375 855917 Fax (+44) 01708202477
HONGERA SANA. NAWAPONGEZA SANA KWA KUJIKWAMUA NA KARAHA HII YA KUBEBA MABOX NA HAWA NDUGU ZETU WA KUTOKEA KULE NANILII KARIBU NA UKRAINE
ReplyDeleteWAZEE WA KAZI.
ReplyDeleteHawa ndio wa kupewa....pacha na sio wale wagaagaa...kutwa kulialia....
ReplyDeletemweusi wa kwanza TILBURY PORT ANAITWA FABIAN(ZIMBWABWE),BUT KEEP IT UP UR DOING GOOD JOOB WAZEE WA KAZI
ReplyDeleteWabongo kwa wivu!! Ndo maana hatuendelei sasa akiwa mzimbabwe sisi tufanye nini??hovyoo!
ReplyDeleteFabian ni half cast wa kizungu
ReplyDeleteBaba yake Fabian ni mzungu muingereza pure aliekwenda Zimbabwe kuwekeza.
Mimi ni mhehe mweusi kama mkaa natokea Kalenga, baba na mama wote wahehe wa Kalenga..
Upo hapo ANONI?