Timu ya mpira wa wavu Mbozi akiwa katika picha kabla ya kupambana na wenzao MUst Mbeya. (picha zote na denis mlowe).

Na Denis Mlowe, Iringa

Makamu Mwenyekiti wa Idara ya michezo ya Halmashauri ya Manispaa Iringa, Kalulu Nsumba ameiomba Serekali pamoja na wadau wa Michezo kusaidia upatikanaji wa vifaa vya mchezo na viwanja bora  ili waweze kuuendeleza mchezo wa Volleball.
 
Nsumba ameyasema hayo katika Bonanza la Mchezo huo lililoandaliwa na na Iringa Manispaa Sport Club lilofanyika kwa siku mbili katika viwanja vya Shule ya sekondari Lugalo na kuzilikisha timu nane za mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya.
 
Amesema mchezo wa volleyball umesaulika na lengo la kuandaa ni kukuza mchezo huo utambulike kama mpira wa miguu na kujenga ushirikiano miongoni mwa vijana wa Nyanda za juu Kusini.
 
 Ameongeza kuwa Nyanda za Juu Kusini kuna vipaji lukuki vya mchezo huo lakini kinachokosekana ni vifaa na viwanja vya mchezo huo na kuwataka wadau kujitokeza kudhamini na kusaida ujenzi wa viwaja bora na kuwataka vijana kujiunga na mchezo huo.
 
Nsumba amedai kuwa kama kutakuwa na ushirikiano wa kutosha na kuwezeshwa kikamilifu mchezo huo kama ilivyo kwa mpira wa miguu anaamini kuwa Iringa na mikoa ya jirani inaweza kuwa na timu zinazoweza kufanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.
 
Alizitaja timu zilizoshiriki bonanza hilo kuwa ni Iringa Manispaa (IMC), Chuo Kikuu cha Iringa (Tumaini), Chuo Kikuu Kishirikishi cha Mkwawa, Must Mbeya, Mbozi Vollebal Club, Tukuyu Volleball Club, Njombe, Ruco na kuwashirikisha vijana zaidi ya 100.
 
Aliwashukuru makampuni ya MT.Huwel, Assas, Meneja wa NBC mkoa wa Iringa na Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa Iringa na shule ya sekondari Lugalo kwa msaada waliotoa kufanikisha bonanza hilo linalotarajiwa kufanyika kila mwaka kwa mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...