Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi wakati alipokuwa anaingi uwanja wa Uhuru leo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar..Pembeni ni Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Joyce Banda wa Malawi katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.Rais Banda kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mfalme MswatiIII katika sherehe za miaka 50 ya Muungano zilizofanyika katika viwanja vya uhuru leo.
Rais dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi katika maadhimisho ya hsrehe za miaka 50 ya Muungano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta katika hsrehe za miaka 50 ya Muungano.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Mohamed Ali Shein na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis
Mwamunyange wakiwa na viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika kwnyesherehe za
Miaka 50 ya Muungano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo. Wengine toka kushoto ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Mfalme Mswati wa III
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal, Mfalme wa Lesotho na rais wa Malawi Dkt Joyce Banda. na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa na viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika kwnyesherehe za Miaka 50 ya Muungano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal, na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakishyangilia kwa furaha wakati Makomandoo wakishuka kwa miavuli uwanjani kama inavyoonekana hapo chini. Mapicha ya kumwaga baadae kidoooogo....
Tuekeeni video ili sisi tuliombali tuone mambo yalivyokuwa-SEOUL. South korea
ReplyDeleteI like that .."The Mighty JWTZ" wamewaonesha hao wanaocheza cheza na Tz kua wakijaribu wataisoma number....nashukuru Kaguta alikuwepo kwani atampelekea salaam PK..na Mama Banda yeye alishudia live..Hongera sana Mh. rais JK kwa kuliongoza taifa letu kwa umakini mkubwa na salaam zingine ziwafikie UKAWA huko waliko kwamba muungano utadumu milele...Ameen.
ReplyDeleteMdau wa UK
MAPINDUZI???? Nilidhani tunaadhimisha Muungano.
ReplyDeleteUSITUCHANGANYE, SHEREHE HII SIYO YA MAPINDUZI NI SHEREHE YA MUUNGANO.
ReplyDeletekweli bwana michuzi tuwekee clip tuone ss tulio mbali
ReplyDeleteTunaomba hotuba ya tarehe 25 na 26 ya mheshimiwa rais jk
ReplyDeleteTunaomba hotuba ya mheshimiwa rais ya muungano na ya tarehe 25
ReplyDeletetunaomba hotuba zote tangu arusha, p.t.a saba saba, na taifa. pls nkali
ReplyDeleteHongera JK kwa kuifikisha TZ yetu halo ilipo na kuwaonesha wale wenye chuki kuwa ukituchezea silaha na vijana wenye ari tunao. Kagame hakuwepo ila nadhani alikuwa anaangalia vijana wenye kofia nyekundu wakifanya maonesho. M23 inawatambua vyema Babu Museveni atakupa taarifa nzuri zaidi
ReplyDeleteTUNAOMBA HOTUBA YA 25TH APR
ReplyDeleteMapidnuzi na Muungano ni kama CHAI NA MKATE!
ReplyDeleteItakuwa kichekesho ukanywa chai bila mkate ama ukala mkate bila kunywa chai!
Ili MUUNGANO upatikane ilitakiwa MAPINDUZI yafanyike kwanza kama tunavyoona ktk Historia Tarehe 12 Januri 1964 MKOLONI WA KIARABU ALIPINDULIWA na ndani ya miezi 3 baadaye Tarehe 26 Aprili, 1964 MUUNGANO ukapatikana.
MUUNGANO HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Ni muhimu waelewe ya kuwa Tanzania siyo nchi ya kuchezea Kijeshi!
ReplyDeleteHiyo MSULI WA MAJESHI ilikuwa ni kama sehemu ya Sherehe tu ktk Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano, na hivyo SINEMA kamili ni pale watakapo fanya nyoko!
ReplyDeleteNi wazi tuna mapungufu kidogo tu katika mambo machache ya ndani ambayo yana rekebishika yakiwemo, Ufisadi, Rushwa na machache yaliyobaki 3 au ma 4 hivi kama Kero za Muungano, LAKINI UWEZO WA KUILINDA NCHI TUNAO.
Cha moto watakiona!