Ndugu zangu Watanzania wa jiji la Houston na vitongoji vyake.Tunapenda kuwatangazia kuwa, kwa kushirikiana na timu ya mpira wa soka ya Houston,tuko mbioni katika kuandaa sherehe za Kumbukumbu ya siku ya Muungano (26/04/1964) uliopelekea kuzaliwa kwa nchi yetu pendwa TANZANIA mnamo tarehe 26 ya mwezi huu wa nne.

Sisi kama Watanzania tunaamini kuwa ni siku hii tukufu inayotupatia UTANZANIA wetu tunaojisifia, kujivunia, na hata kuupigania kote ulimwenguni.

Tafadhali rejea kiambata hapo chini kwa maelezo na maelekezo ya ziada.

Tutawaletea taarifa zaidi kama zitakavyojiri, na tunaomba mawazo, ushauri,na ushiriki wenu pale muonapo inastahiki kufanya hiyvo ili kuboresha shughuli yetu hii.

Tunatanguliza shukrani zetu kwenu nyote.

Imetolewa kwa niaba ya Uongozi wenu na:
SAIDI M. NUSURA
AFISA MAWASILIANO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Asante sana Saidi.Tuulinde Muungano wetu,Uwe wa serikali X,Y,Z, nk suala muhimu ni kutouvunja muungano wetu Nukta

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...