Na ticha Yusuph Kileo.
Katika Muendelezo wa Kuelimisha Jamii jinsi ya kubaki salama mitandaoni, leo najikita katika maswala ya USIRI (PRIVACY) ambapo taarifa nyingi za mtu binafsi si vyema kuwekwa mitandaoni na pia maelezo mafupi ya namna wahalifu mtandao wanatumia taarifa hizo za siri mitandaoni kuleta madhara.
Njia za awali ambazo wahalifu mtandao wanatumia kabla ya kusababisha madhara ni kukusanya taarifa za mhusika ambaye wanategemea kumdhuru kwa njia inayojulikana kitaalam kama “RECONNAISSANCE” ambapo mara nyingi taarifa za awali zinapatikana kwenye mitandao ya kijamii kwani inaaminika wengi hawana umakini katika kutoa taarifa zao kupitia mitandao ya kijamii.
Jamii inashauriwa kujenga umakini wa taarifa binafsi wanazo
ziweka mitandaoni ili kuweza kubaki salama. “Takwimu inaonyesha asilimia kubwa
ya watumiaji wamekuwa wakiweka taarifa ambazo zinaweza kutoa urahisi wakugundua
mambo mengi kutoka kwa muhusika” – Yusuph Kileo.
Mfano, Kuna wale ambao hadi leo wanatumia maneno ya siri
“PASSWORDS” kwa kutumia mwaka wao wa kuzaliwwa wakati kuo huo mwaka huo wa
kuzaliwa umewekwa kwenye mitandao ya kijamii hapo inaonyesha ni jinsi gani
muhusika huyu anatengeneza urahisi kwa mhalifu kuweza kumuingilia kumdhuru.
Aidha, Umuhimu mkubwa unahitajika katika utoaji wa siri za
mtu binafsi kwani panapokua na ugumu katika kukusanya taarifa za awali za mtu
binafsi kunajengeka ugumu wa ukusanyaji wa taarifa za muhusika ambapo kunapelekea
ugumu kwa mhalifu kuleta madhara kirahisi kwa mhusika.
Pia Kumekua na wimbi la wahalifu wanao omba moja kwa moja
kupitia baruapepe au mitandao ya kijamii taarifa za watu na takwimu zinaonyesha
kuna wale ambao bado wanatoa taarifa hizo bila kujua athari zake.
“Nashauri Unapo pokea jumbe inayo kuhitaji utoe taarifa zako
binafsi aidha kwa maelezo kuwa kuna matengenezo katika akaunti yako au
kukuwezesha kifedha na kuanzisha uhusiano kuwa makini kwani ni moja ya hatua za
ukusanyaji wa taarifa za mtu ili kujenga njia ya kuanzisha madhara”
Picha: inaonyesha mambo ya msingi kuzingatia utumiapo
mitandao ya kijamii ili kuweza kujenga ugumu kwa wahalifu mtandao kuleta
madhara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...