MTENDAJI MKUU WA WAKALA WA BARABARA TANZANIA (TANROADS) ANAPENDA KUTOA TAARIFA KWA UMMA NA WATUMIA BARABARA YA BAGAMOYO – MAKOFIA - MSATA KWAMBA BARABARA HII IMEFUNGWA KWA AJILI YA USALAMA WA ABIRIA NA VYOMBO VYA USAFIRI KUTOKANA NA MVUA KUBWA ZINAZONYESHA NCHINI NA KULETA MAFURIKO KWENYE BONDE LA DARAJA LA RUVU CHINI.
MADEREVA WANASHAURIWA KUTUMIA BARABARA YA DAR ES SALAAM – CHALINZE - MOROGORO NA BAGAMOYO – MLANDIZI – CHALINZE KWA KIPINDI HIKI AMBACHO BARABARA YA BAGAMOYO – MAKOFIA – MSATA IMEFUNGWA.
TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA NA ASANTE KWA USHIRIKIANO.
IMETOLEWA NA,
MTENDAJI MKUU – WAKALA WA BARABARA
P.O BOX 11364
3RD FLOOR
AIRTEL BUILDING
ALI HASSAN MWINYI/ KAWAWA ROADS JUNCTION
DAR ES SALAAM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...