Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF , Bwana Ladislaus Mwamanga akiwatambulisha baadhi ya wageni walioshiriki katika kikao cha kujifunza kutoka kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini katika shehia ya Mwembemakumbi wilaya ya Mjini Unguja ambako ujumbe huo umekuweko kwa siku Tatu.
Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF Bwana Amedius Kamagenge akitoa ufafanuzi wa moja ya masuala yaliyojitokeza katika kikao cha pamoja kati ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini katika shehia ya Mwembemakumbi wilaya ya Mjini Unguja na wadau wa maendeleo ambao wamefanya ziara ya siku TATU kisiwani Unguja.
Baadhi ya wajumbe kutoka nchi wafadhili waliohudhuria kikao cha walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika shehia ya Mwembemakumbi wilaya ya Mjini Unguja wakisikiliza maoni kutoka kwa walengwa wa mpango huo (hawapo pichani) Nyuma ni Meneja wa Fedha wa TASAF Bwana Nyamuko na Meneja Ukaguzi wa TASAF Bwana Mziray wakifuatilia mjadala huo.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya kusimamia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika Shehia ya Mwembemakumbi ,wilaya ya Mjini Unguja akitoa ufafanuzi wamaswali yaliyobuliwa na baadhi ya wajumbe kutoka nchi wafadhili wa mpango huo juu ya namna walengwa wa mpango huo walivyopatikana.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bwana Ladislaus Mwamanga (mwenye sharti la draft) akiwa na wageni kutoka nchini Marekani wakimsikiliza mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (hayupo pichani ) katika shehia ya Mwembemakumbi wakati alipotoa hoja zake juu ya manufaa ya Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF.
.Mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini katika shehia ya Mwembemakumbi ,wilaya ya Mjini Unguja akitoa mawazo yake juu ya namna Mpango huo unavyomunufaisha.
Baadhi ya wajumbe wa nchi wafadhili na viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wakielekea kwenye ukumbi ambako wamekutana na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika shehia ya MwembeMakumbi wilaya ya Mjini Unguja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...