Na: Geofrey Tengeneza – Abuja Nigeria
Jumuiya ya wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi wa Nigeria kwa ujumla, wameombwa kuja kuwekeza kwa ujumla na kutembelea vivutio vya utalii mbalimbali vinavyopatikana nchini Tanzania.
Hayo yamesemwa na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay katika maadhimisho ya miaka hamsini 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) yalioandaliwa na ofisi ya ubalozi waTanzania nchini Nigeria na kufanyika katika Hoteli ya Sheraton jijini Abuja.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa kongamano hili la Biashara na Uwekezaji, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay amesema Tanzania inajivunia muungano wake ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa la Tanzania Mwl Julius Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume muasisi wa Zanzibar mnamo tarehe 26 April, 1964 ambao sasa umetimia miaka 50.
“Watanzania tunajivunia sana muungano wetu kwani ni wa kipekee sana hapa barani Afrika, na ni muungano uliodumu kwa muda mrefu zaidi kuliko muungano wowote ule Barani Afrika”…alisema Balozi Njoolay.
Akizungumzia kuhusu fursa za biashara Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa TANTRADE Bwana Edwin Rutageruka amesema kwamba mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizi mbili yameendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na kwamba Tanzania imedhamiria kuendelea kukuza biashara kati yake na Nigeria.
Naye Mkurugenzi wa mipango na maendeleo wa mamlaka ya EPZ Bwana Lamau Mpolo ameelezea uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo ya gesi na madini. Ameelezea pia namna serikali ya Tanzania ilivyoweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuvutia wawekezaji kutoka duniani kote katika sekta mbalimbali za uchumi nchini Tanzania.
Akiwasilisha mada kuhusu vivutio vya utalii vya Tanzania vilivyomo katika orodha ya maajabu ya 7 ya asili barani Africa, Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB Bibi Teddy Mapunda amesema pamoja na vivutio vitatu (3) vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Crater ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi zaidi na vya kipekee na akabainisha kuwa imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutangaza vivutio vyake saba vya asili ambavyo pamoja na vile vilivyomo katika maajabu Saba ya sili barani Afrika, vivutio vingine ni hifadhi ya taifa ya Ruaha, Hifadhi ya Taifa ya Kituro, hifadhi ya Taifa ya Gombe na Pori la akiba la Selous.
Amewakaribisha wananchi wa Nigeria kutembelea Tanzania na kujionea uzuri na upekee wa vivutio vya Tanzania.
Kongamano hilo lililohudhuriwa na takribani wawekezaji na wafanyabiasha kutoka Nigeria mia moja lilifuatiwa na tafrija iliyofanyika usiku katika hoteli hiyo na kuhuidhuriwa na waalikwa takribani 350 wakiwemo Mabalozi wa mataifa mbalimbali nchi Nigeria, wageni kadhaa mashuhuri na baadhi ya watanzania waishio nchini Nigeria.
Balozi wa Tanzania chini Nigeria Mh. Daniel Ole Njoolay akifungua kongamano la Biashara na uwekezaji katika Hoteli ya Serena jijini Abuja Nigeria ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizoandaliwa na ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB Bibi Teddy Mapunda akizungumza wakatio Alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu vivutio vya utalii vta Tanzania katika kongamano la biashara na uwekezaji jijini Abija nchini Nigeria.
Mh. Daniel Ole Njoolay, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria akikata keki huku akishuhudiwa na mwakilishi wa wa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan (wa pili kulia) na baadhi mabalozi wanaowakilisha nchi zao Nigeria katika tafrija iliyotayarishwa na ubalozi wa Tanzania kusherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika hotel ya Serena jijini Abuja Nigeria.
Kikundi cha ngoma za asili cha Abuja Nigeria kikitoa burudani ya ngoma katika tafrija kusheherekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika hoteli ya Serena jijini Abuja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...