Kenny Mwangoka akiendesha gari hilo ambalo bodi lake limetengenezwa kwa mbao

Kenny Mwangoka akifungua mlango wa nyuma wa gari hilo akionesha umadhubuti wa bori lake

Mwanahabari huyu Oliva Motto wa Star TV hakuamini kama kilichounda bodi ya gari hilo ni mbao mpaka alipogusa na kujiridhisha

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Peter Tweve akimpongeza Mwangoka kwa ubinifu huo

Na Francis Godwin, Iringa

Amini usiamin. Bodi la gari hili aina ya Hiace lenye namba za usajili T921 BME limetengenezwa kwa mbao aina ya mlingoti na pine. Linamilikiwa na mvunaji na mfanyabishara wa mbao wa Nyololo, Mafinga, mkoani Iringa Bw.Kenny Mwangoka.

Mwangoka alilinunua gari hilo lililokuwa linamilikiwa na mission ya kanisa katoliki Mafinga baada ya kupata ajali na kuharibika vibaya. Jitihada zake za kulifufua gari hilo kwa kuvisha bodi mpya hazikuzaa matunda na ndipo alipotumia ubunifu huu.

"Mimi mwenyewe ni fundi wa magari, kwahiyo kazi ya kuunda na kuvisha bodi hili la mbao nilifanya mwenyewe," anasema, na kuongeza kuwa baada ya matengenezo hayo gari hilo limekuwa kivutio kikubwa sehemu mbalimbali anazopita nalo.

"Sasa nalitumia kuhamasisha utalii, hasa utalii wa mazingira nikiwa na maana kwamba tukiyatunza mazingira yatatufaa kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na matengenezo ya magari kama hili langu," anasema, na kuongeza kuwa  atalipeleka kwenye maonesho ya nanenane mwaka huu kama moja ya njia za kuhamasisha upandaji wa miti. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ila tu ndugu Mwangoka usipakie abiria kama daladala maana viwango kwa usafiri wa abiria bado.

    Gari ipigongwa kidogo vibande vya 'kuni' au' mbao' vitakuwa hatarishi mara mia kuliko bodi ya aluminiamu maana aluminiami hubonyea au kupinda lakini mbao vitaruka vipande vipande na kuleta madhara makubwa kwa abiria.

    ReplyDelete
  2. Are you really serious? I wouldn't risk my life. Is it insured?

    ReplyDelete
  3. Usalama vipi hapo? bodi za magari ni scientifically proved na zina viwango kwa kuzingatia mambo mengi sanaa achana na ajali hata upepo etc...kuna sababu lukuku za bodi za magari kuwa na shepu au kuwa na materials fulani sio just tu kujiwekea kitu chochote...pia kuna kuzingatia hali ya hela etc..mambo ni mengi..wataalamu wa TBS wameruhusi hili?..sipingi ubunifu na kama lina viwango vyote na TBS wameruhusu basi mie nampongeza sana huyu bwana....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...