Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari hawapo pichani kuhusu Rasimu ya Katiba ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Simba baada ya wanahabari kutaka kupata ufafanuzi juu ya hatma ya Katiba na uchaguzi wa Klabu hiyo.
Na: Genofeva Matemu
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imemaliza kupitia
Rasimu ya Katiba ya Club ya Simba kwa ajili ya kuidhinisha katiba hiyo na kuifanya
Club ya Simba kuendelea na taratibu za uchaguzi mkuu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Bw. Leonard Thadeo alipokutana na waandishi wa habari kujibu hoja
mbalimbali za waandishi leo jijini Dar es Salaam.
Akijibu moja ya hoja iliyomtaka kufafanua Wizara imefikia wapi katika upatikanaji wa
Katiba ya Club ya Simba Bw. Thadeo amesema kuwa upitiaji wa Katiba umemelizika
na kuonekana kuwa na mapungufu machache yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara
iweze kuidhinisha katiba hiyo.
“Mchakato wa upitiaji wa Katiba ya Club ya Simba umemalizika jana lakini
kumekuwepo na mapungufu machache yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara iweze
kuidhinisha Katiba hiyo” amesema Bw. Thadeo.
Akifafanua zaidi Bw. Thadeo amesema kuwa mapungufu hayo yanalenga zaidi upande
wa kisheria ambapo mtu anaweza kutafsiri neno vibaya hivyo kupata maana tofauti
na Katiba ilivyokusudia hivyo kuitaka Club hiyo kufanya marekebisho hayo mapema na
kurejesha Katiba hiyo Wizarani kwa ajili ya kuidhinishwa.
Aidha Bw. Thadeo amewataka waandishi wa habari pamoja na wanachama wa Club
ya Simba kuwa na subira ili waweze kupata Katiba itakayokidhi malengo ya Club yao
kwani mchakato wa upitiaji wa Katiba ulihitaji umakini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...